Usanidi wa Printa

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Usanidi wa Printa

Mip'o Chanzo Karatasi:
Mipangilio ya Karatasi:

Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyoingiza katika chanzo cha karatasi.

A4/Letter Ubad. Ot.:

Teua Washa Ili kuweka karatasi kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa A4 wakati hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa kama Letter, au huweka kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa Letter ambapo hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa A4.

Ilani ya Hitilafu:

Teua Washa ili kuonyesha ujumbe wa kosa wakati ukubwa wa karatasi ulioteuliwa haufanani na karatasi iliyopakiwa.

Ony. Ot. Usan'i/ Kar.:

Chagua Washa ili kuonyesha skrini ya Mipangilio ya Karatasi unapopakia kwenye kaseti ya karatasi. Ukilemaza kipengele hiki, huwezi kuchapisha kutoka kwenye iPhone, iPad au iPod touch ukitumia AirPrint.

Hali Tulivu:

Teua Washa ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji. Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi.

Kipima Saa ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

Mip'ilio ya Kuzima:

Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.

  • Zima Ikiwa Haitumiki

    Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.

  • Zima ikiwa Imetenganishwa

    Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.

    Angalia tovuti ifuatayo kwa muda maalum.

    https://www.epson.eu/energy-consumption

Lugha/Language:

Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.

Kibodi:

Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.

Kipima saa cha Kulala:

Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.

Muda wa Kukausha Wino:

Teua muda wa kukausha wino unaotaka kutumia unapotekeleza uchapishaji wa pande 2.Kichapishi huchapisha upande mwingine baada ya kuchapisha upande mmoja.Iwapo chapisho lako limepakwa wino, ongeza mpangilio wa muda.

Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB:

Teua Wezesha ili kuruhusu kompyuta kufikia kichapishi inapounganishwa kwenye USB. Wakati Lemaza imeteuliwa, uchapishaji na utambazaji ambao haujatumwa kupitia muunganisho wa mtandao unazuiwa.