Unaweza kuangalia au kubadilisha ukubwa na aina ya karatasi kwenye skrini inayoonyeshwa unapochomeka kaseti ya karatasi. Iwapo utasajili ukubwa na aina ya karatasi, kichapishi kinakujulisha ikiwa maelezo yaliyosajiliwa na mipangilio ya chapisho ni tofauti. Hii hukuzuia kupoteza karatasi na wino kwa kuhakikisha kwamba huchapishi kwenye ukubwa usiofaa wa karatasi au kuchapisha kwa rangi isiyofaa kutoka na kutumia mipangilio ambayo hailingani na aina ya katarasi.

Iwapo ukubwa wa karatasi unaoonyeshwa ni tofauti na karatasi iliyopakiwa, teua Badilisha ili kufanya mabadiliko. Teua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi, angalia mipangilio, na kisha ubonyeze kitufe cha OK. Iwapo mipangilio inalingana na karatasi iliyopakiwa, teua Thibitisha.
Iwapo hutaki kuonyesha skrini ya mpangilio wa karatasi kiotomatiki unapochomeka kaseti ya karatasi, kwenye skrini ya nyumbani teua Mipangilio > Usanidi wa Printa > Mip'o Chanzo Karatasi > Ony. Ot. Usan'i/ Kar., na kisha uteue Zima.