Unaweza kutumia mbinu zozote kati ya zifuatazo kutambaza ukitumia kichapishi hiki.
Kuna mbinu mbili za kutambaza nakala asili kwa kompyuta; kutambaza ukitumia paneli dhibiti ya kichapishi na kutambaza kutoka kompyuta.
Unaweza kutambaza kwa urahisi kutoka katika paneli dhibiti. Baada ya kutambaza, sakinisha Epson Event Manager na Epson Scan 2 kwenye kompyuta yako.
Tumia programu ya utambazaji Epson ScanSmart ili kutambaza kutoka kompyuta. Unaweza kuhariri taswira baada ya kutambaza. Kabla ya kutambaza, sakinisha Epson ScanSmart kwenye kompyuta yako.
Unaweza kuhifadhi picha iliyotambazwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi, kwa kutumia kipengele cha WSD.
Iwapo unatumia Windows 7/Windows Vista, unahitaji kuunda mipangilio ya WSD kwenye kompyuta yako kabla ya kutambaza.
Unaweza kuhifadhi taswira zilizotambazwa moja kwa moja kwenye kifaa maizi kama vile smartphone au kompyuta kibao kwa kutumia programu ya Epson iPrint kwenye kifaa maizi.
Kabla ya kutambaza, sakinisha Epson iPrint kwenye kifaa chako maizi.