Teua Matengenezo kwenye skrini ya nyumbani.
Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya
, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.
Teua Jaza Wino.
Bonyeza kitufe cha
ili kuhamisha tanki la wino hadi mkao wa kujaza.
Bonyeza kitufe cha
ili kusoma tahadhari zote za usalama na matumizi kwa kujaza wino, na kisha ubonyeze kitufe cha OK ili kuendelea.
Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa.

Fungua kifuniko cha tanki la wino.

Unaposhikilia chupa ya wino wima, geuza kifuniko polepole ili kukiondoa.

Epson inapendekeza utumie chupa halali za wino za Epson.
Chunga usimwage wino wowote.
Usiguse upande wa juu wa chupa ya wino baada ya kuondoa kifuniko; vinginevyo unaweza kujipaka wino.

Angalia mstari wa juu (a) kwenye tanki la wino.

Pangilia upande wa juu wa chupa ya wino kwa kituo cha kujaza, na kisha uichomeke wima kwenye kituo cha kujaza wino kwenye mstari wa juu.
Wino utaanza kumwagika na mtiririko utakoma kiotomatiki wakati wino umefikia mstari wa juu.
Iwapo wino hautaanza kutiririka kwenye tanki, ondoa chupa ya wino na ujaribu kuichomeka tena. Hata hivyo, usichomeke upya chupa ya wino wakati wino umefika mstari wa juu; vinginevyo wino unaweza kuvuja.

Usiruhusu sehermu ya juu ya chupa ya wino kugonga vifaa vyovyote baada ya kuondoa kifuniko; vinginevyo wino unaweza kumwagika.
Unapokamilisha kujaza wino, ondoa chupa ya wino.
Usiache chupa ya wino kama imechomekwa; vinginevyo huenda chupa ikaharibika au wino unaweza kumwagika.
Iwapo wino wowote utasalia kwenye chupa ya wino, kaza kifuniko na uhifadhi cvhupa ikisimama kwa matumizi ya baadaye.

Funga kifuniko cha tanki la wino.

Bonyeza kitufe cha
, kisha ufuate maagizo ya kwenye askrini ili kuweka kiwango cha wino.
Hata kama hutajaza wino hadi mstari wa juu wa tanki la wino, unaweza kuendelea kutumia kichapishi. Ili kufanya kichapishi chako kiendelee kufanya kazi kwa hali nzuri, hata hivyo, jaza upya tanki la wino hadi mstari wa juu na kisha uweke upya viwango vya wino mara moja.
Funga kitengo cha kitambazaji.