Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:
Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na urefu wa karatasi.
Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Mipangilio inayopatikana inalinganana aina ya karatasi unayoteua. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.
Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.
Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha.
Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya mpangilio wa muundo ili kubainisha utaratibu ambao kurasa zinachapishwa.
Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.
Huchapisha nyaraka nyingi zilizolinganishwa kwa utaratibu na kupangwa kwenye vikundi.
Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.
Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.
Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.