Unapounganisha kompyuta kwenye kichapishi kwa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) ukitumia Mtandao kupitia mawasiliano ya data ya simu ya kasi ya chini, huenda usiweze kufikia Mtandao kwa sababu kichapishi kina muunganisho wa kipaumbele. Fuata hatua zilizo hapa chini ili kupunguza kipaumbele kwa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) na kuongeza kipaumbele kwa mawasiliano ya data ya simu.
Onyesha skrini ya Windows ya muunganiso wa mtandao.
Teua Muunganisho wa Mtandao Pasiwaya (DIRECT-XXXXXXXX), bofya kulia ili kuonyesha menyu, na kisha uteue Sifa.
Teua Toleo la Itifaki ya Mtandao 4 (TCP/IPv4) au Mtandao, na kisha ubofye Sifa.
Iwapo unatumia Windows Vista au la baadaye kwa IPv6, teua Toleo la Itifaki ya Mtandao 6 (TCP/IPv6).
Bofya Mahiri.
Futa Metriki otomatiki, na kisha uingize “100” kwenye Metriki ya kiolesura.
Bofya Sawa ili kufunga dirisha.