Jaribu suluhu zifuatazo.
Hakikisha kuwa kitovu kimewashwa.
Washa upya kitovu (zingatia watumiaji wengine ambao huenda wanatumia mtandao). Subiri takriban dakika moja baada ya kuwasha upya kitovu, na kisha uangalie tena muunganisho.
Hakikisha kuwa kebo ya Ethaneti imeunganishwa salama. Iwapo mwangaza wa hali ya muunganisho umezima, angalia mwangaza wa hali kwa kuunganisha kituo kingine au kubadilisha kebo ya Ethaneti. Iwapo hili halitatatua tatizo, badilisha kitovu.
Washa upya kichapishi. Utaratibu ambao kichapishi na kitovu vinawashwa unaweza kusababisha kosa la muda la muunganisho. Subiri takriban dakika moja baada ya kuwasha upya kichapishi, na kisha uangalie tena muunganisho.
Ikiwa kuna mgogoro wa anwani ya IP, muunganisho wa mtandao unaweza kutokuwa thabiti au kutopatikana. Angalia anwani ya IP kwa kila kifaa na utoe anwani za kipekee za IP.
Iwapo ulibadilisha modi ya muunganisho kutoka kwenye Wi-Fi hadi kwenye Ethaneti, unahitaji kulemaza Wi-Fi ili kuwezesha Ethaneti. Lemaza Wi-Fi kwenye kidirisha cha kudhibiti cha kichapishi.
Unapotumia Ethaneti, huenda kichapishi na kitovu visiunganishwe iwapo modi yake ya muunganisho haiwiani. Tazama yafuatayo kwa maelezo ya michanganyijo ya modi inayopatikana.
Kitovu |
||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Otomatiki |
1000Base-T Sehemu Mbili Kamili |
1000Base-T Sehemu Mbili Nusu |
100Base-TX Sehemu Mbili Kamili |
100Base-TX Sehemu Mbili Nusu |
10Base-T Sehemu Mbili Kamili |
10Base-T Sehemu Mbili Nusu |
||
Kichapishi |
Otomatiki |
✓ |
✓ |
✓ |
– |
✓ |
– |
✓ |
100Base-TX Sehemu Mbili Kamili |
– |
– |
– |
✓ |
– |
– |
– |
|
100Base-TX Sehemu Mbili Nusu |
✓ |
– |
– |
– |
✓ |
– |
– |
|
10Base-T Sehemu Mbili Kamili |
– |
– |
– |
– |
– |
✓ |
– |
|
10Base-T Sehemu Mbili Nusu |
✓ |
– |
– |
– |
– |
– |
✓ |
Unaweza kubadilisha modi ya munganisho kwa kutumia EpsonNet Config au Web Config. Iwapo huna EpsonNet Config, ipakue kutoka kwenye tovuti ifuatayo ya Epson.
http://www.epson.eu/Support (Ulaya)
http://support.epson.net/ (nje ya Ulaya)