Kusajili Kichapishi kwenye Google Cloud Print (Kutumia Web Config)

Ili kutumia huduma hii, unahitaji akaunti ya Google. Iwapo huna akaunti ya Google, unahitaji kufungua moja kwanza.

http://www.google.com/cloudprint/learn/

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Angalia anwani ya IP ya kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP kwa kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.

    Kumbuka:

    Iwapo unataka kujua maelezo ya IPv6, chapisha laha la hali ya mtandao.

  3. Endesha kivinjari cha Wavuti kutoka kwenye kompyuta au kifaa maizi, na kisha uingize anwani ya IP ya kichapishi.

    Umbizo:

    IPv4: http://anwani ya IP ya kichapishi/

    IPv6: http://[anwani ya IP ya kichapishi]/

    Mifano:

    IPv4: http://192.168.100.201/

    IPv6: http://[2001:db8::1000:1]/

    Kumbuka:
    • Unapofikia Web Config kupitia HTTPS, ujumbe wa tahadhari utaonekana kwenye kivinjari kwa kuwa cheti kilichotiwa sahihi kibinafsi, kilichohifadhiwa kwenye kichapishi, kinatumika.

    • Ukitumia kifaa mahiri, unaweza pia kuendesha Web Config katika skrini ya matengenezo Epson iPrint.

    Mfano ni kurasa zifuatazo. Kwa maelezo, tazama Mwongozo wa Mtumiaji au Mwongozo wa Msimamizi (inapatikana tu kwa modeli maalum) kwa bidhaa yako.

  4. Bofya au donoa Firmware Update, na kisha ufuate maagizo ili kusasisha programu dhibiti ya kichapishi.

    Wakati huwezi kubofya au kudonoa Firmware Update, bofya Administrator Login na kisha uingize kwanza nenosiri.

  5. Bofya au donoa Google Cloud Print Services.

  6. Bofya au donoa Register.

  7. Bofya au donoa Usage Advisory, yasome kwa uangalifu na uyaklubali, kisha ubofye au kudonoa Next.

    Skrini ya uthibitisho inaonyeshwa.

  8. Bofya au donoa OK ili kufungua skrini ya usajili wa Google Cloud Print.

  9. Ingga kwenye Google kwa kutumia akaunti yako.

  10. Bofya au donoa kitufe cha usajili kwenye tovuti ya Google.

    Wakati usajili unakamilika, laha la maelezo limechapishwa kutoka kwa kichapishi ulichosajili. Sasa unaweza kutumia huduma ya Google Cloud Print.

    Ili kutumia huduma hii, teua menyu ya uchapishaji kutoka kwenye programu-tumizi tangamanifu ya Google Cloud Print.

    Kumbuka:
    • Unaweza kufikia ukurasa wa udumishaji wa Google Cloud Print kwa kuingia kwenye Google na kufikia ukurasa wa mipangilio ya akaunti.

    • Kwa maelezo kuhusu Google Cloud Print, tazama msaada kwa Google Cloud Print kwenye tovuti ya Google.

    • Iwapo unataka kuhairisha au kuendelea na huduma ya Google Cloud Print au iwapo unataka kufuta kichapishi kilichosajiliwa, unda mipangilio kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi au kutoka Web Config. Kwa maelezo zaidi, tazama nyaraka ya kichapishi.