Iwapo kichapishi chako tayari kinaonyeshwa kwenye Vichapishi na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume faksi), teua kichapishi chako, na ubofye kitufe cha – ili kufuta. Ongeza kiendeshi cha kichapishi na kiendeshi cha faksi (kwa modeli zilizo na kitendaji cha faksi) kulingana na maagizo yaliyo hapa chini.
Teua menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishi na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume faksi).
Bofya kitufe cha +.
Teua Ongeza Kichapishi au Kitambazaji.
Teua kichapishi cha Epson kutoka kwenye orodha.
Teua kiendeshi kilichotaka kichapishi chako.
Angalia jedwali lililo hapa chini, ili kuhakikisha umeteua sahihi.
Mbinu ya Muunganisho |
Kiendeshi cha Kichapishi |
Kiendeshi cha Faksi |
---|---|---|
USB |
EPSON XXXXX |
FAX XXXXX (USB) |
Mtandao |
EPSON XXXXX EPSON XXXXX -YYYYYY |
FAX EPSON XXXXX (IP) FAX EPSON XXXXX -YYYYYY (IP) FAX ZZZ.ZZZ.ZZZ.ZZZ (IP) |
* XXXXX = Jina la bidhaa. YYYYYY = Anwani ya MAC dijiti 6. ZZZ.ZZZ.ZZZ.ZZZ = Anwani ya IP.
Bofya Ongeza.
Pindi unapoongeza kiendeshi (viendeshi), huhitaji kuviongeza tena isipokuwa ubadilishe mbinu yako ya muunganisho au utumie bidhaa tofauti. Hakikisha bidhaa imewashwa na kuunganishwa vilivyo kwenye kompyuta yako kwa kutumia muunganisho wa USB au mtandao. Inaweza kuchukua muda kutafuta kiendeshi cha faksi. Subiri hadi kiendeshi cha faksi kionyeshwe kwenye orodha, na kisha uongeze kiendeshi cha faksi kwa kutumia utaratibu sawa.