Unaweza kutumia amri ya Ping ili kuhakikisha kompyuta imeunganishwa kwenye kichapishi.Fuata hatua zilizo hapa chini ili kuangalia muunganisho kwa kutumia amri ya Ping.
Angalia anwani ya IP kwa muunganisho ambao unataka kuangalia.
Unaweza kuangalia hii kutoka kwenye skrini ya Hali ya Mtandao kwenye kidirisha cha kudhibiti kichapishi, ripoti ya muunganisho, au safuwima ya IP Address ya jedwali la hali ya mtandao.
Onyesha skrini ya swali la amri ya kompyuta.
Weka “ping xxx.xxx.xxx.xxx”, kisha ubonyeze kitufe cha Enter.
Weka anwani ya IP ya kichapishi ya xxx.xxx.xxx.xxx.
Angalia hali ya mawasiliano.
Ikiwa kichapishi na kompyuta vinawasiliana, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.
Ikiwa kichapishi na kompyuta havinawasiliani, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.