Jaribu suluhu zifuatazo.
Angalia iwapo mipangilio ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi) simewezeshwa kwenye kichapishi.
Angalia iwapo nywila ya muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) imebadilishwa. Unaweza kuiangalia kwenye paneli dhibiti ya kichapishi (inapatikana tu kwa modeli maalum) au laha la hali ya mtandao.
Angalia ikiwa kichapishi kimezimwa. Ikiwa umeweka kipima muda cha kuzima kawi kwenye kichapishi, kichapishi kinazimika kiotomatiki baada ya muda fulani.
Kwa mtumiaji wa Android, iwapo huwezi kuunganisha kwenye kichapishi kutoka kwenye kifaa maizi kwa kutumia muunganisho wa Wi-Fi Direct hata iwapo hali ya muunganisho [Imealikwa] kwenye kifaa maizi, huenda kifaa kimesajiliwa kama kifaa kilichokataliwa kwenye kichapishi. Weka upya maelezo yaliyosajiliwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi au Web Config. Kitendaji hiki hufuta maelezo yote ya kifaa kilichosajiliwa.