Kusakinisha Programu ya Ziada — Windows

EPSON Software Updater husakinisha programu ya ziada. Inaweza pia kusasisha programu thabiti ya kichapishi na programu iliyosakinishwa pia.

Kumbuka:

Iwapo EPSON Software Updater haijasakinishwa, fikia tovuti ifuatayo.

http://epson.sn

Ingiza jina la bidhaa, nenda kwenye Mpangilio, na kisha ubofye Pakua ili kupakua kisakinishaji. Bofya au bofya mara mbili faili iliyopakuliwa ili kuendesha kisakinishaji. Iwapo skrini ya Teua Usakinishaji wa Programu imeonyeshwa, teua Sakinisha programu-tumizi na kisha ubofye Ifuatayo.

  1. Tekeleza EPSON Software Updater.

    • Windows 10
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu zote > Epson Software > Epson Software Updater.
    • Windows 8.1/Windows 8
      Ingiza jina la programu-tumizi katika sehemu ya utafutaji, na kisha uteue ikoni iliyoonyeshwa.
    • Windows 7/Windows Vista/Windows XP
      Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote (au Programu) > Epson Software > Epson Software Updater.
  2. Teua jina la programu unayotaka kusakinisha kutoka kwenye orodha ya sasa ya programu, kisha usakinishe.

    Kumbuka:

    Iwapo unatumia bidhaa nyingi, tafadhali teua majina ya modeli. Orodha inaonyesha majina ya programu iliyosasishwa na programu ambayo inayosambazwa kutoka kwenye tovuti.