Kuongeza Kompyuta ya Kuunganisha — Mac OS X

Pakua programu kutoka kwenye tovuti, kisha ufanye muunganisho wa mipangilio kwa kuongeza kompyuta. Utaratibu huu unafafanuliwa kwenye hali ambayo kichapishi tayari kimeunganishwa kwenye mtandao, na kompyuta unayotaka kuongeza imeunganishwa kwenye SSID sawa.

Kumbuka:

Maudhui yanayoonyeshwa kwenye skrini hutofautiana kulinagana na modeli na hali.

  1. Fikia tovuti ifuatayo kutoka kwenye kompyuta unayotaka kuunganisha kwenye kichapishi, kisha uingize jina la bidhaa.

    http://epson.sn

  2. Nenda kwenye Mpangilio.

  3. Bofya Pakua ili kupakua kisakinishaji.

  4. Endesha kisakinishaji kwa kubofya au kubofya mara mbili faili ya kupakua.

  5. Bofya mara mbili ikoni ifuatayo.

  6. Angalia makubaliano ya leseni na ubofye Next.

  7. Teua programu ya kusakinisha na ubofye Install.

    Epson Network Utilities na Epson Driver and Utilities lazima iteuliwe.

    Usakinishaji wa programu unaanza.

  8. Teua Additional Computer kwenye skrini ifuatayo.

    Fuata maagizo ya kwenye skrini.