Unaweza kutumia amri ya Ping ili kuhakikisha kompyuta imeunganishwa kwenye kitambazaji. Fuata hatua zilizo hapa chini ili kuangalia muunganisho kwa kutumia amri ya Ping.
Angalia anwani ya IP ya kitambazaji kwa muunganisho ambao unataka kuangalia.
Unaweza kuangalia hii kwa kutumia Epson Scan 2.
Tekeleza Matumizi ya Mtandao.
Weka “Matumizi ya Mtandao” katika Spotlight.
Bofya kichupo cha Ping, weka anwani ya IP uliyoangalia katika hatua ya 1, kisha ubofye Ping.

Angalia hali ya mawasiliano.
Ikiwa kitambazaji na kompyuta vinawasiliana, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.

Ikiwa kitambazaji na kompyuta haviwasiliani, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.
