Kuunganisha kwenye Kompyuta kupitia Ethaneti — Mac OS X

Unaweza kusanidi kiotomatiki muunganisho wa Ethaneti kati ya kitambazaji na kompyuta kwa kutumia kisakinishaji.

Kumbuka:

Maudhui yanayoonyeshwa kwenye skrini hutofautiana kulinagana na modeli na hali.

  1. Fikia tovuti ifuatayo kutoka kwenye kompyuta unayotaka kuunganisha kwenye kitambazaji, kisha uingize jina la bidhaa.

    http://epson.sn

  2. Nenda kwenye Mpangilio.

  3. Bofya Pakua ili kupakua kisakinishaji.

  4. Endesha kisakinishaji kwa kubofya au kubofya mara mbili faili ya kupakua.

  5. Bofya mara mbili ikoni ifuatayo.

  6. Angalia makubaliano ya leseni na ubofye Next.

  7. Teua programu ya kusakinisha na ubofye Install.

    Epson Network Utilities na Epson Driver and Utilities lazima iteuliwe.

    Usakinishaji wa programu unaanza.

  8. Teua Ethernet Network Connection kwenye skrini ifuatayo.

    Fuata maagizo ya kwenye skrini.