Kuangalia Muunganisho kwa Kutumia Amri ya Ping — Windows

Unaweza kutumia amri ya Ping ili kuhakikisha kompyuta imeunganishwa kwenye kitambazaji. Fuata hatua zilizo hapa chini ili kuangalia muunganisho kwa kutumia amri ya Ping.

  1. Angalia anwani ya IP ya kitambazaji kwa muunganisho ambao unataka kuangalia.

    Unaweza kuangalia hii kwa kutumia Epson Scan 2.

  2. Onyesha skrini ya swali la amri ya kompyuta.

    • Windows 10
      Bofya kulia kitufe cha kuwasha au bonyeza na ukishikilie, na kisha uteue Kisituo cha Amri.
    • Windows 8.1/Windows 8
      Onyesha skrini ya programu, kisha uteue Swali la Amri.
    • Windows 7 au awali
      Bofya kitufe cha kuanza, teua Programu Zote au Programu > Vifuasi > Swali la Amri.
  3. Weka “ping xxx.xxx.xxx.xxx”, kisha ubonyeze kitufe cha Enter.

    Weka anwani ya IP ya kitambazaji ya xxx.xxx.xxx.xxx.

  4. Angalia hali ya mawasiliano.

    Ikiwa kitambazaji na kompyuta vinawasiliana, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.

    Ikiwa kitambazaji na kompyuta haviwasiliani, ujumbe ufuatao unaonyeshwa.