Kuweka Paneli Dhibiti

Usanidi wa paneli dhibiti ya kichapishi. Unaweza kusanidi kama ifuatavyo.

  1. Fikia Web Config na uteue kihupo cha Device Management > Control Panel.

  2. Weka vipengee vifuatavyo inavyohitajika.

    • Language
      Teua lugha iliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti.
    • Operation Timeout
      Iwapo utateua ON, unapoingia kama mtumiaji wa kudhibiti ufikiaji au msimamizi, unaondolewa kiotomatiki na kuenda kwenye skrini ya mwanzo iwapo hakuna shughuli kwa kipindi fulani cha muda.
      Unaweza kuweka kati ya sekunde 10 na dakika 240 kulingana na sekunde.
    Kumbuka:

    Unaweza pia kuweka mipangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    • Language: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Lugha/Language

    • Operation Timeout: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Muda wa Shughuli Umeisha (Unaweza kubainisha Kuwasha au Kuzima).

  3. Bofya OK.