Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:
Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo Ukubwa wa Waraka inatofautiana na Karatasi ya Zao, Punguza/Kuza Waraka inateuliwa kiotomatiki. Huhitaji kuiteua unapochapisha bila kupunguza au kuongeza ukubwa wa waraka.
Hukuruhusu kupunguza au kuongeza ukubwa wa waraka.
Punguza au ongeza ukubwa wa waraka kiotomatiki ili utoshee ukubwa wa karatasi iliyoteuliwa kwenye Karatasi ya Zao.
Huchapisha kwa asilimia maalum.
Huchapisha picha katikati ya karatasi.
Hurekebisha rangi za picha kiotomatiki.
Hukuruhusu ili kutekeleza urekebishaji wa rangi kikuli. Kubofya Iliyoboreshwa hufungua skrini ya Usahihishaji wa Rangi ambapo unaweza kuchagua mbinu ya kina ya urekebishaji wa rangi. Hukuruhusu kuweka mbinu ya Chapisho Lote la Rangi ili kukoleza matini na mistari unapobofya Chaguo za Taswira. Pia unaweza kuwezesha Ula'aji wa Pambizo, Rkbsha Jicho Jekundu, na mipangilio ya uchapishaji ya kupungua kwa kufifia kwa kingo.
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa ruwaza za kutonakili, taswira fifi, au vijajuu na vijachini.
Hukuruhusu kuongeza au kuondoa ruwaza zozote za kutonakili na nakala au taswira fifi unazotaka kutumia.
Hukuruhusu kuweka mbinu ya uchapishaji kwa ruwaza za kutonakili au taswira fifi.
Unaweza kuchapisha maelezo kama vile jina la mtumiaji na tarehe ya kuchapisha kwenye vijajuu na vijachini. Kisha unaweza kuweka rangi, fonti, ukubwa au muundo.
Huzungusha kurasa nyuzi 180 kabla ya kuchapisha. Teua kipengee hiki unapochapisha kwenye karatasi kama vile bahasha zilizopakiwa katika mwelekeo thabiti kwenye kichapishi.
Huchapisha wakati kichwa cha kuchapisha kinasogea pande zote mbili. Kasi ya uchapishaji na haraka, lakini ubora unaweza kupungua.
Hugeuza picha ili iweze kuchapisha kama vile ingeonekana kwenye kioo.