Kuunda Mipangilio ya Kutuma na Kupokea Faksi kwenye Kompyuta

Ili kutuma na kupokea faksi kwenye kompyuta, FAX Utility inafaa kusakinishwa kwenye kompyuta iliyounganishwa kwa mtandao au kebo ya USB.

Kuwezesha Kutuma Faksi kutoka kwenye Kompyuta

Weka mipangilio ya yafuatayo ukitumia Web Config.

  1. Fikia Web Config, bofya kichupo cha Fax na kisha ubofye Send Settings.

  2. Teua Use kwa ajilil ya PC to FAX Function.

    Thamani chaguomsingi ya PC to FAX Function ni Use. Ili kulemaza utumaji faksi kutoka kwenye kompyuta yoyote, teua Do Not Use.

  3. Bofya OK.

Kufanya Mpangilio wa Hifadhi kwenye Kompyuta Kupokea Faksi

Unaweza kupokea faksi kwenye kompyuta kwa kutumia FAX Utility. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta na kuunda mpangilio. Kwa maelezo, tazama Basic Operations kwenye msaada wa FAX Utility (yanayoonyeshwa kwenye dirisha kuu).

Kipengee kilicho hapa chini cha mpangilio kwenye paneli dhibiti ya kichapishi kimewekwa kwa Ndiyo, na faksi zilizopokewa zinaweza kuhifadhiwa kwenye kompyuta.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea > Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta

Kufanya Mpangilio wa Hifadhi kwenye Kompyuta ili Pia Kuchapisha kwenye Kichapishi ili Kupokea Faksi

Unaweza kuunda mpangilio ili kuchapisha faksi zilizopokewa kwenye kichapishi na pia kuzihifadhi kwenye kompyuta.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Teua Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta > Ndiyo na Uchapishe.

Kuunda Mpangilio wa Hifadhi kwenye Kompyuta Kutopokea Faksi

Ili kuweka kichapishi kutopokea faksi kwenye kompyuta, badilisha mipangilio kwenye kichapishi.

Kumbuka:

Pia unaweza kubadilisha mipangilio kwa kutumia FAX Utility. Hata hivyo, iwapo kuna faksi zozote ambazo hazijahifadhiwa kwenye kompyuta, kipengele hakifanyi kazi.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani kwenye paneli dhibiti.

  2. Teua Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea.

  3. Teua Faksi Towe > Hifadhi kwenye Kompyuta > La.