CA-signed Certificate
Hiki ni cheti ambacho kimetiwa sahihi na CA (Mamlaka ya Cheti). Unaweza kukipata ili kukitumia kwa Mamlaka ya Cheti. Cheti hiki kinathibitisha kuwepo kwa kichapishi na kinatumika kwa mawasiliano ya SSL/TLS ili uweze kuhakikisha usalama wa mawasiliano ya data.
Cheti cha CA
Hiki ni cheti ambacho kiko katika msururu wa CA-signed Certificate, pia kinajulikana kama cheti cha kati cha CA. Kinatumika na kivinjari ili kuidhinisha njia ya cheti cha kichapishi wakati wa kufikia seva ya mhusika mwingine au Usanidi za Wavuti.
Kwa cheti cha CA, weka wakati wa kuidhinisha njia ya cheti cha seva kwa kufikia kutoka kwenye kichapishi. Kwa kichapishi, weka kuidhinisha njia ya CA-signed Certificate kwa muunganisho wa SSL/TLS.
Unaweza kupata cheti cha CA cha kichapishi kutoka kwa Mamlaka ya Utoaji Cheti ambapo cheti cha CA kinatolewa.
Pia, unaweza kupata cheti cha CA kilichotumika kuidhinisha mhusika mwingine kutoka kwa Mamlaka ya cheti kilichotoa CA-signed Certificate ya seva nyingine.
Self-signed Certificate
Hiki ni cheti ambacho kichapishi hutia sahihi na kutoa chenyewe. Pia kinajulikana kama cheti msingi. Kwa sababu mtoaji anakiidhinisha, haiwezi kutegemewa na haiwezi kuzuia kuiga.
Kitumie unapofanya mipangilio ya usalama na kutekeleza mawasiliano rahisi ya SSL/TLS bila CA-signed Certificate.
Ukitumia cheti hiki kwa mawasiliano ya SSL/TLS, arifa ya usalama inaweza kuonyeshwa kwenye kivinjari cha wavuti kwa sababu cheti hakijasajiliwa kwenye kvinjari cha wavuti. Unaweza kutumia Self-signed Certificate pekee kwa mawasiliano ya SSL/TLS.