Mipangilio ya Kutuma

Unaweza kupata menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kutuma

Kumbuka:

Kwenye skrini ya Web Config, unaweza kutafuta menyu hapa chini.

Kichupo cha Fax > Send Settings

Kuzungushwa Otomatiki:

Hati halisi yenye ukubwa A4 iliyowekwa katika ADF au kwenye glasi ya kichanganuzi yenye mpaka wake mrefu ukiangalia kushoto hutumwa kama faksi yenye ukubwa wa A3. Wezesha hii ili uzungushe picha iliyochanganuliwa ili kuituma kwa ukubwa wa A4.

Muda wa Kusubiri wa Asili Ifuatayo:

Weka muda wa kusubiri nakala asili ifuatayo. Kichapishi huanza kutuma faksi baada ya muda kupita.

Muda wa Uonyesho Kuhak'i Faksi:

Unaweza kuhakiki waraka uliotambazwa kwa mara kadhaa kabla ya kuutuma. Kichapishi huanza kutuma faksi baada ya muda kupita.

Ukubwa Asili Uteuzi (ADF):

Hii inapowezeshwa na unapakia nakala asili kwenye ADF inayozidi upana wa laha ya karatasi ya taswira ya A4, unaweza kuteua ukubwa wa waraka unaofaa kutumwa na faksi.

PC to FAX Function:

Kipengee hiki kinaonyeshwa kwenye skrini ya Web Config pekee. Huwezesha utumaji faksi kwa kutumia kompyuta ya mteja.