> Utambazaji > Inatambaza Nakala Asili hadi kwenye Kabrasha ya Mtandao > Chaguo za Menyu za Kutambaza kwa Utambazaji kwenye Kabrasha

Chaguo za Menyu za Kutambaza kwa Utambazaji kwenye Kabrasha

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Eneo la Kutambaza:

Teua eneo la kutambaza. Ili kupuna nafasi nyeupe kwenye matini au taswira unapotambaza, teua Upunuaji Otomatiki. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua Upeo wa Eneo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Hali ya Rangi:

Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika monokromu.

Umbizo la Faili:

Teua umbizo ambalo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.

Unapotaka kuhifadhi kama PDF, PDF/A au TIFF, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).

  • Mgao wa Mfinyazo:

    Teua kiwango cha kufinyaza picha iliyotambazwa.

  • Mipangiliuo ya PDF:

    Unapoteua PDF kama mpangilio wa kuhifadhi umbizo, tumia mipangilio hii kulinda faili za PDF.

    Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kufungua, weka Nenosiri la Kufungua Hati. Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kuchapisha au kuhariri, weka, Nenosiri la Vibali.

Ubora
  • Mwonekano:

    Teua mwonekano wa utambazaji.

  • Aina ya Hati:

    Teua aina ya nakala yako asili.

Pande 2:

Tambaza pande zote za nakala asili.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

  • Ufungaji(Asili):

    Teua mwelekeo wa kuweka pamoja wa nakala asili.

Mwelekeo (Asili):

Teua mwelekeo wa nakala asili.

Uzito:

Teua ulinganuzi wa taswira iliyotambazwa.

Ondoa Kivuli:

Ondoa vivuli vya nakala asili ya ambavyo vinaonekana katika taswira iliyotambazwa.

  • Mzunguko:

    Ondoa vivuli katika ukingo wa nakala asili.

  • Katikati:

    Ondoa vivuli vya pambizo za kuweka pamoja vya kijitabu.

Ondoa Mashimo ya Panchi:

Ondoa mashimo ya panji ambayo yanaonekana kwenye taswira iliyotambazwa. Unaweza kubainisha eneo la kufuta mashimo ya panji kwa kuingiza thamani kwenye kikasha upande wa kulia.

  • Mkao wa Kufuta:

    Teua mkao ili kuondoa mashimo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Jina la Faili:
  • Kiambishi awali cha Jina la faili:

    Ingiza kiambishi awali cha jina la taswira katika vibambo vya alfanumeriki na alama.

  • Ongeza Tarehe:

    Ongeza tarehe ya jina la faili.

  • Ongeza Muda:

    Ongeza muda kwenye jina la faili.

Ondoa Mipangilio Yote

Rejesha mipangilio ya kutambaza kuwa chaguomsingi.