Upangaiji wa Anwani ya IP

Hizi ni aina zifuatazo za upangaiji wa anwani ya IP.

Anwani Thabiti ya IP:

Pangia anwani ya IP iliyothibitishwa awali kwenye kichapishi (kipangaji) kikuli.

Maelezo ya kuunganisha kwenye mtandao (barakao ya mtandao mdogo, kichanganishi njia chaguo-smingi, seva ya DNS na kadhalika) yanahitaji kuwekwa kikuli.

Anwani ya IP haibadiliki wakati kifaa kimezimwa, kwa hivyo hii ni muhimu unapotaka kudhibiti vifaa kwa mazingira ambayo huwezi kubadilisha anwani ya IP au unataka kudhibiti vifaa kwa kutumia anwani ya IP. Tunapendekeza mipangilio kwenye kichapishi, seva, nk, ambayo kompyuta nyingi hufikia.

Upangiaji otomatiki kwa kutumia kitendaji cha DHCP (anwani inayobadilika ya IP):

Pangia anwani ya IP kiotomatiki kwenye kichapishi (kipangaji) kwa kutumia kitendaji cha DHCP cha seva au kipanga niia cha DHCP.

Maelezo ya kuunganisha kwenye mtandao (barakao ya mtandao mdogo, kichanganishi njia chaguo-msingi, seva ya DNS na kadhalika) imewekwa kiotomatiki, kwa hivyo unaweza kuunganisha kifaa kwenye mtandao kiurahisi.

Iwapo kifaa au kipanga njia kimezimwa, au kulingana na mipangilio ya seva ya DHCP, anwani ya IP inaweza kubadilisha wakati wa kuunganisha upya.

Tunapendekeza kudhibiti vifaa kando na anwani ya IP na kuwasiliana na itifaki zxinazoweza kufuata anwani ya IP.

Kumbuka:

Unapotumia kitendaji cha kuhifadhi nafasi cha anwani ya IP cha DHCP, unaweza kupangia anwani ya IP sawa kwenye vifaa wakati wowote.