Sanidi hii unapotaka kutumia kitendaji cha utambazaji kwa kutumia barua pepe.
Angalia yafuatayo kabla ya kusanidi.
Kichapishi kimeunganishwa kwenye mtandao unaoweza kufikia seva ya barua.
Maelezo ya mipangilio ya barua pepe ya kompyuta ambayo hutumia seva ya barua sawa na ya kichapishi.
Unapotumia seva ya barua kwenye Mtandao, thibitisha maelezo ya mipangilio kutoka kwenye mtoa huduma au tovuti.
Fikia Web Config na uteue kichupo cha Network > Email Server > Basic.
Ingiza thamani kwa kila kipengee.
Teua OK.
Mipangilio ambayo umeteua inaonyeshwa.
Usanidi unapokamilika, fanya ukaguzi wa muunganisho.