Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Eneo la Kutambaza:
Teua eneo la kutambaza. Ili kupuna nafasi nyeupe kwenye matini au taswira unapotambaza, teua Upunuaji Otomatiki. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua Upeo wa Eneo.
Mwelekeo (Asili):
Teua mwelekeo wa nakala asili.
Nyeusi na Nyeupe/Rangi
Chagua ikiwa utatambaza kwenye monokromu au kwa rangi.
Umbizo la Faili:
Teua umbizo ambalo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.
Unapotumia PDF kama ubizo la faili, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).