> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Huhifadhi trei towe.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Mwongozo kwa Aikoni ya Mtandao

Huonyesha skrini ya Mipangilio ya Sauti ya Kifaa. Unaweza kuweka Nyamazisha na Hali Tulivu. Pia unaweza kufikia menyu ya Sauti kutoka kwenye skrini. Unaweza pia kuweka mipangilio hii kutoka kwenye menyu ya Mipangilio.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Sauti

Huonyesha iwapo Hali Tulivu imewekwa kwa kichapishi au la. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho.

Huonyesha kuwa Nyamazisha imewekwa kwa kichapishi.

Huonyesha orodha ya mipangilio iliyosajiliwa kwenye Iliyowekwa mapema.

Pia unaweza kusajili mipangilio pendwa mipya.

Huonyesha skrini ya Maelezo ya Data ya Faksi. Nambari inayoonyeshwa inaashiria idadi ya faksi ambazo bado hujasoma, kuchapisha au kuhifadhi.

Huonyesha kila menyu.

  • Nakili

    Hukuruhusu kunakili nyaraka.

  • Changanua

    Hukuruhusu kutambaza nyaraka au picha na kuzihifadhi kwenye kompyuta.

  • Faksi

    Hukuruhusu kutuma faksi.

  • Matengenezo

    Huonyesha menyu zinazopendekezwa kuimarisha ubora wa machapisho yako kama vile kuzibua nozeli kwa kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli na kutekeleza usafishaji wa kichwa, na kuboresha ukungu au mistari kwenye machapisho yako kwa kupangilia kichwa cha kuchapisha. Unaweza pia kuweka mipangilio hii kutoka kwenye menyu ya Mipangilio.

    Mipangilio > Matengenezo

  • Mipangilio

    Hukuruhusu kuweka mipangilio inayohusiana na udumishaji, mipangilio ya kichapishi na operesheni.

Hutelezesha skrini upande wa kulia.