Ufafanuzi huu ni mfano wa kuunda kabrasha lililoshirikiwa lililo kwenye eneo-kazi la mtumiaji anayeingia kwenye kompyuta.
Mtumiaji anayeingia kwenye kompyuta na aliye na mamlaka ya msimamizi anaweza kufikia kabrasha la eneo kazi na kabrasha la waraka lililo chini ya kabrasha la Mtumiaji.
Weka usanidi huu wakati HUMRUHUSU mtumiaji mwingine kusoma au kuandika kwenye kabarasha lililoshirikiwa lililo kwenye kompyuta ya kibinafsi.
Mahali pa kuunda kabarasha lililoshirikiwa: Eneo-kazi
Njia ya kabrasha: C:\Users\xxxx\Desktop\scan_folder
Idhini ya ufikiaji kupitia mtandao (Idhini za Kushiriki): Kila mtu
Idhini ya ufikiaji kwenye mfumo wa faili (Usalama): usiongeze, au kuongeza majina ya Mtumiaji/Kikundi ili kutoa idhini
Ingia kwenye kompyuta ambapo kabrasha lililoshirikiwa litakapoundwa na akaunti ya mtumiaji wa mamlaka ya msimamizi.
Washa kichunguzi.
Unda kabrasha kwenye eneo-kazi kisha ulipe jina “scan_folder”.
Kwa jina la kabrasha, ingiza vibambo kati ya 1 na 12 vya herufi na tarakimu. Iwapo utazidi kikomo cha idadi cha jina la kabrasha, huenda usiweze kulifikia kikawaida katika mazingira anuwai.
Bofya kulia kwenye kabrasha, na kisha uteue Sifa.

Bofya Kushiriki Mahiri kwenye kichupo cha Kushiriki.

Teua Shiriki kabarasha hili, na kisha ubofye Idhini.

Teua Kila mtu kikundi cha Kikundi au majina ya watumiaji, teua Ruhusu kwenye Mabadiliko, na kisha ubofye OK.

Bofya OK.
Teua kichupo cha Usalama.
Angalia kikundi au mtumiaji kwenye Kikundi au majina ya mtumiaji.
Kikundi au mtumiaji anayeonyeshwa hapa anaweza kufikia kabrasha lililoshirikiwa.
Katika hali hii, mtumiaji anaingia kwenye kompyuta hii na Msimamizi anaweza kufikia kabrasha lililoshirikiwa.
Ongeza idhini ya ufikiaji, ikiwa ni muhimu. Unaweza kuiongeza kwa kubofya Hariri. Kwa maelezo zaidi, tazama Maelezo Husiani.

Teua kichupo cha Kushiriki.
Njia ya mtandao ya kabrasha lililoshirikiwa inaonyeshwa. Hii inatumika wakati wa kusajili kwenye waasiliani wa kichapishi. Tafadhali inakili.

Bofya OK au Funga ili kufunga skrini.
Bofya ikiwa faili inaweza kuandikwa au kusomwa kwenye kabrasha lililoshirikiwa kutoka kwenye kompyuta za watumiaji au vikundi vilivyo na idhini ya ufikiaji.