Unaweza kulemaza kiolesura kinachotumika kuunganisha kifaa kwenye kichapishi. Weka mipangilio ya vizuizi ili kuzuia uchapishaji na utambazaji kwa njia tofauti na kupitia mtandao.
Pia unaweza kuweka mipangilio ya vizuizi kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Muungan. Kompyuta kupitia USB: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Muungan. Kompyuta kupitia USB
Fikia Web Config na uteue kihupo cha Product Security > External Interface.
Teua Disable kwenye vitendaji unavyotaka kuweka.
Teua Enable unapotaka kughairi udhibiti.
Muungan. Kompyuta kupitia USB
Unaweza kuzuia matumizi ya muunganisho wa USB kutoka kwenye kompyuta. Iwapo unataka kuyazuia, teua Disable.
Bofya OK.
Hakikisha kwamba kituo kilicholemazwa hakiwezi kutumika.
Muungan. Kompyuta kupitia USB
Iwapo kiendeshi kimesakinishwa kwenye kompyuta
Unganisha kichapishi kwenye kompyuta ukitumia kebo ya USB, na kisha uthibitishe kwamba kichapishi hakichapishi.
Iwapo kiendeshi hakijasakinishwa kwenye kompyuta
Windows:
Fungua kidhibiti cha kifaa na ukidumishe, unganisha kichapishi kwenye kompyuta ukitumia kebo ya USB kisha uthibitishe kwamba maudhui ya kuonyeshwa kwenye kidhibiti cha kifaa yanasalia bila kubadilishwa.
Mac OS:
Unganisha kichapishi kwenye kompyuta ukitumia kebo ya USB, na kisha uthibitishe kwamba kichapishi hakijaorodheshwa iwapo unataka kuongeza kichapishi kutoka kwenye Vichapishi na Vitambazaji.