Kubadilisha Vibweta vya Wino

Wakati ujumbe unaonyeshwa ukikusitua kubadilisha vibweta vya wino, teua Jinsi ya na kisha utazame uhuishaji ulioonyeshwa kwenye paneli dhibiti ili kujifunza jinsi ya kubadilisha vibweta vya wino.

Iwapo unahitaji kubadilisha vibweta vya wino kabla ya kutanuliwa, teua Mipangilio > Matengenezo > Ubadilishaji wa Kibweta cha Wino kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, na kisha ufuate maagizo ya kwenye skrini. Teua Jinsi ya kwa maelezo.

Tahadhari:

Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.