Kuleta cheti kilichotiwa Sahihi cha CA

Leta CA-signed Certificate ulichopata kwenye kichapishi.

Muhimu:
  • Hakikisha mpangilio wa tarehe na saa wa kichapishi ni sahihi. Huenda cheti si halali.

  • Ukipata cheti ukitumia CSR iliyoundwa kutoka kwa Web Config, unaweza kuleta cheti mara moja.

  • Unapoleta CA-signed Certificate kwa kuteua kichupo cha Network Security > S/MIME > Client Certificate, huwezi kubadilisha Sender's Email Address kwenye kichupo cha Network > Email Server > Basic. Iwapo unataka kubadilisha Sender's Email Address, badilisha mipangilio yote ya cheti kuwa Do not add signature kwa kuteua kichupo cha Network Security > S/MIME > Basic kisha ufute cheti cha kuletwa cha CA-signed Certificate.

  1. Fikia Web Config, kisha uteue kichupo cha Network Security.

  2. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • SSL/TLS > Certificate
    • IPsec/IP Filtering > Client Certificate
    • IEEE802.1X > Client Certificate
    • S/MIME > Client Certificate
  3. Bofya Import.

    Ukurasa wa kuleta cheti unafunguliwa.

  4. Ingiza thamani kwa kila kipengee. Weka CA Certificate 1 na CA Certificate 2 unapothibitisha njia ya cheti kwenye kivinjari cha wavuti kinachofikia kichapishi.

    Kwa kutegemea unapoundia CSR na umbizo la faili la cheti, mipangilio inayohtajika inaweza kutofautiana. Ingiza thamani kwa vipengee vinavyohitajika kulingana na yafuatayo.

    • Cheti cha umbizo la PEM/DER kilichopatikana kutoka Web Config
      • Private Key: Usisanidi kwa sababu kichapishi kina ufunguo wa kibinafsi.
      • Password: Usisanidi.
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Cha hiari
    • Cheti cha umbizo la PEM/DER kilichopatikana kutoka kwenye kompyuta
      • Private KeyUnhitaji kuweka.
      • Password: Usisanidi.
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Cha hiari
    • Cheti cha umbizo la PKCS#12 kilichopatikana kutoka kwenye kompyuta
      • Private Key: Usisanidi.
      • Password: Cha hiari
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Usisanidi.
  5. Bofya OK.

    Ujumbe wa kukamilisha unaonyeshwa.

Kumbuka:

Bofya Confirm ili uthibitishe maelezo ya cheti.