Vipengee Vinavyoweza Kuwekwa Kibinafsi

Msimamizi anaweza kuruhusu vipengee kuonyeshwa na kubadilisha mipangilio kibinafsi.

  • Ufikiaji wa kumbukumbu ya Kazi: Kazi/Hali > Kumbukumbu

    Dhibiti onyesho la hali ya historia ya kazi ya kiwambo. Teua Washa ili kuruhusu historia ya kazi kuonyeshwa.

  • Fikia ili uweze Kuwasajili/Kuwafuta Waasiliani: Mipangilio > Kisimamia Waasiliani > Ongeza/Hariri/Futa

    Dhibiti usajili na kubadilika kwa waasiliani. Teua Washa ili kusajili au kubadilisha waasiliani.

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Faksi: Faksi > Mpokeaji > Hivi karibuni

    Dhibiti onyesho la mafikio unapotuma na kupokea faksi. Teua Washa ili kuonyesha mafikio.

  • Ufikiaji wa Batli ya Usambazaji Faksi: Faksi > Menyu > Kumbukumbu ya Upitishaji

    Dhibiti onyesho la historia ya mawasiliano ya faksi. Teua Washa ili kuonyesha historia ya mawasiliano.

  • Ufikiaji wa Ripoti ya Faksi: Faksi > Menyu > Ripoti ya Faksi

    Dhibiti uchapishaji wa ripoti ya faksi. Teua Washa ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Kuh. Cha. kwa Folda/FTP ya Mt'o: Changanua > Folda/FTP ya Mtandao > Menyu > Chapisha Historia ya Kuhifadhi

    Dhibiti uchapishaji wa historia ya kuhifadhi kwa kutambaza kwenye kitendaji cha kabrasha la mtandao. Teua Washa ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Changanua kwa Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Mpokeaji > Historia

    Dhibiti onyesho la historia kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua Washa ili kuonyesha historia.

  • Ufikiaji wa Onyesha Historia ya Zilizotumwa ya Changanua kwa Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Menyu > Onyesha Historia ya Kutuma

    Dhibiti onyesho la historia ya kutuma barua pepe kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua Washa ili kuonyesha historia ya kutuma barua pepe.

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Zilizotumwa ya Changanua kwa Barua pepe: Changanua > Barua pepe > Menyu > Chapisha Historia ya Kutuma

    Dhibiti uchapishaji wa historia ya kutuma barua pepe kwa kutambaza kwenye kitendaji cha barua. Teua Washa ili kuruhusu uchapishaji.

  • Ufikiaji wa Lugha: Mipangilio > Lugha/Language

    Dhibiti mabadiliko ya lugha inayoonyeshwa kwenye paneli dhibiti. Teua Washa ili kubadilisha lugha.

  • Ufikiaji wa Karatasi Nyembamba: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Karatasi Nyembamba

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Karatasi Nyembamba. Teua Washa ili kubadilisha mipangilio.

  • Ufikiaji wa Hali Tulivu: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Hali Tulivu

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Hali Tulivu. Teua Washa ili kubadilisha mipangilio.

  • Ufikiaji wa Kipaumbele cha Kasi ya Kuchapisha: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Ki'bele cha Kasi ya Uc'pishaji

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Ki'bele cha Kasi ya Uc'pishaji. Teua Washa ili kubadilisha mipangilio.

  • Ufikiaji wa Kugundua Uwekaji Mara Mbili: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Gundua Uwekaji Mara mbili

    Dhibiti mabadiliko ya mipangilio ya kitendaji cha Gundua Uwekaji Mara mbili. Teua Washa ili kubadilisha mipangilio.

  • Ulinzi wa Data ya Kibinafsi:

    Dhibiti onyesho la maelezo ya mafikio kwenye usajili wa upigaji haraka. Teua Washa ili kuonyesha mafikio kama (***).

  • Ruhusu Ufikiaji wa Trei ya Towe ya Kunakili: Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Printa > Towe: Nakala

    Dhibiti mabadiliko ya mahali pa towe unaponakili. Teua Washa ili kubadilisha mipangilio.

  • Kubali Zima Nishati:

    Dhibiti kibali cha kuzima kichapishi. Teua Washa ili kuiruhusu kuzima.