Kichupo cha Kuu

Uwekaji Kabla Uchapishaji:

Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:

Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.

Viwango vya Wino:

Huonyesha kiwango kinachokadiriwa cha wino. Unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki. Unaweza kuipakua kutoka kwenye tovuti ya Epson.

Onyesha Mipangilio/Ficha Mipangilio:

Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.

Rejesha Chaguo-msingi:

Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi pia hurejeshwa katika chaguomsingi zao.

Uhakiki wa Chapisho:

Huonyesha uhakiki wa waraka wako kabla ya kuchapisha.

Laiti ya Kipangaji cha Kazi:

Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.

Chanzo cha K'tasi:

Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Teua Uteuzi Otomatiki ili kuteua kiotomatiki chanzo cha karatasi kilichoteuliwa kwenye mipangilio ya kichapishi.

Ukubwa wa Waraka:

Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na kimo cha karatasi kisha usajili ukubwa.

Karatasi ya Zao:

Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo Ukubwa wa Waraka inatofautiana na Karatasi ya Zao, Punguza/Kuza Waraka inateuliwa kiotomatiki. Huhitaji kuiteua unapochapisha bila kupunguza au kuongeza ukubwa wa waraka.

Punguza/Kuza Waraka:

Hukuruhusu kupunguza au kuongeza ukubwa wa waraka.

Tosheleza kwenye Ukurasa:

Punguza au ongeza ukubwa wa waraka kiotomatiki ili utoshee ukubwa wa karatasi iliyoteuliwa kwenye Karatasi ya Zao.

Kuza hadi:

Huchapisha kwa asilimia maalum.

Katikati:

Huchapisha picha katikati ya karatasi.

Aina ya Krtasi:

Teua aina ya karatasi unayochapisha. Iwapo utateua Teua Otomatiki (karatasi wazi), uchapishaji unatelezwa kutoka kwa chanzo cha karatasi ambapo aina ya karatasi imewekwa kwa ifuatayo kwenye mipangilio ya kichapishi.

Karatasi tupu, Preprinted, Letterhead, Rangi, Recycled, Karatasi wazi la ubora wa juu

Hata hivyo, karatasi haliwezi kuingizwa kutoka kwenye chanzo ambacho chanzo cha karatasi kimewekwa kwa zima kwenye Mipangilio ya Uchaguaji Oto cha kichapishi.

Ubora:

Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Mipangilio inayopatikana inalinganana aina ya karatasi unayoteua. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.

Taarifa ya Chanzo cha Karatasi:

Huonyesha maelezo ya karatasi iliyowekwa kwa kila chanzo cha karatasi.

Mwelekeo:

Teua mwelekeo unaotaka kutumia ili kuchapisha.

Rangi:

Teua iwapo utachapisha kwenye rangi au katika monokromu.

Uchapishaji wa Pande 2:

Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.

Settings:

Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha. Unapochapisha nyaraka za kurasa nyingi, unaweza kuteua kuchapisha kuanzia upande wa mbele au upande wa nyuma wa ukurasa.

Uzito wa Uchapishaji:

Teua aina ya waraka ili kurekebisha uzito wa chapisho. Iwapo uzito wa chapisho unaofaa umeteuliwa, unaweza kuzuia picha kutokea upande wa nyuma. Chagua Mwenyewe ili urekebishe uzito wa chapisho wewe mwenyewe.

Kurasa Nyingi:

Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya mpangilio wa muundo ili kubainisha utaratibu ambao kurasa zinachapishwa.

Mpangilio Kinyume:

Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.

Pangiliza/Zisizopangwa:

Teua Pangiliza ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi zilizochanganywa kwa mpangilio na kupangwa kwenye vikundi.

Copies:

Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.