> Kukarabati Kichapishi > Kubadilisha Kibiringiza cha Matengenezo kwenye Mkanda 1 wa Karatasi

Kubadilisha Kibiringiza cha Matengenezo kwenye Mkanda 1 wa Karatasi

Kuna maeneo mawili ya kubadilisha kibiringiza cha matengenezo: upande wa nyuma wa kichapishi (rola mbili) na kwenye mkanda wa karatasi (rola moja).

  1. Zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha , na kuondoa plagi kwenye kamba ya nishati.

  2. Ondoa kibiringiza cha matengenezo mpya kutoka kwenye kifurushi chake.

    Muhimu:
    • kibiringiza cha matengenezo ya mkanda 1 wa karatasi na mkanda 2 hadi 4 wa karatasi ni tofauti. Angalia mwelekeo wa kishale upande wa katikati wa kibiringiza cha matengenezo, na uhakikishe kibiringiza cha matengenezo ni za mkanda 1 wa karatasi. Iwapo utaambatisha rola zisizo sahihi, huenda kichapishi kisiingize karatasi.

    • Kuwa makini usikwaruze au kuweka mado ya kibiringiza cha matengenezo. Iwapo vumbi litakusanywa kwenye eneo la kibiringiza cha matengenezo, safisha rola kwa kutumia kitambaa laini na kilicho na unyevu. Kutumia kitambaa kilichokauka kunawea kuharibu eneo la rola.

  3. Vuta mkanda 1 wa karatasi.

  4. Geuza kichapishi, na ufungue kifuniko 1 cha nyuma.

  5. Vuta kifuniko 2 cha nyuma.

  6. Ondoa kifuniko ndani ya upande wa nyuma wa kichapishi.

  7. Telezeshesha kibiringiza cha matengenezo viwili vilivyotumiwa,na uviondoe.

  8. Chomeka kibiringiza cha matengenezo mbili mpya hadi zitoshee katika eneo.

    Kumbuka:

    Chomeka kibiringiza cha matengenezo kwa kuzizungusha ili uweze kuchomeka vizuri.

  9. Funika tena kifukinu ndani ya upande wa nyuma wa kichapishi.

  10. Chomeka kifuniko 2 cha nyuma.

  11. Funga kifuniko 1 cha nyuma.

  12. Achilia wenzo wa mkanda wa karatasi.

  13. Telezesha kibiringiza cha matengenezo kwenye wenzo, na kisha uziondoe kwa kuchukua shafti ya kishikio.

  14. Chomeka shafti ya kibiringiza cha matengenezompya kwenye shimo kwenye kishikio, na kisha utelezeshe shafti kwenye upande wa wenzo kwenye mpenyo wakati inaangalia eneo bapa upande wa mbele.

  15. Funga wenzo.

  16. Chomeka mkanda wa karatasi.

  17. Washa kichapishi, teua Mipangilio > Matengenezo > Maelezo ya Rola ya Matengenezo > Weka upya Kaunta ya Rola ya Matengenezo, na kisha uteue mkanda wa karatasi ambapo ulibadilisha kibiringiza cha matengenezo.