Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa:
Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.
Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye kichupo cha Kuu pia hurejeshwa katika chaguomsingi zao.
Teua Kazi ya Siri ili uweke nenosiri la kulinda nyaraka za siri unapochapisha. Iwapo utatumia kipengele hiki, data ya kuchapisha inahifadhiwa kwenye kichapishi na inaweza kuchapishwa tu baada ya nenosiri kuingizwa kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi. Bofya Mipangilio ya Kazi ya Siri ili kubadilisha mipangilio.
Hurekebisha rangi za picha kiotomatiki.
Hukuruhusu ili kutekeleza urekebishaji wa rangi kikuli. Kubofya Iliyoboreshwa hufungua skrini ya Urekebishaji wa Rangi ambapo unaweza kuchagua mbinu ya kina ya urekebishaji wa rangi. Bofya Chaguo za Taswira ili kuwasha Chapisho Lote la Rangi, Rkbsha Jicho Jekundu, na ukuze uchapishaji wa laini nyembamba.
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa ruwaza za kutonakili, taswira fifi, au vijajuu na vijachini.
Hukuruhusu kuongeza au kuondoa ruwaza zozote za kutonakili na nakala au taswira fifi unazotaka kutumia.
Hukuruhusu kuweka mbinu ya uchapishaji kwa ruwaza za kutonakili au taswira fifi.
Unaweza kuchapisha maelezo kama vile jina la mtumiaji na tarehe ya kuchapisha kwenye vijajuu na vijachini.
Huzungusha kurasa nyuzi 180 kabla ya kuchapisha. Teua kipengee hiki unapochapisha kwenye karatasi kama vile bahasha zilizopakiwa katika mwelekeo thabiti kwenye kichapishi.