Usimamizi wa Mtandao

Kwa kutumia menyu hii, unaweza kudumisha bidhaa kama msimamizi wa mfumo. Pia hukuruhusu kuzuia vipengele vya bidhaa kwa watumiaji binafsi ili kukidhi kazi yako au mtindo wa ofisi.

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao

Kisimamia Waasiliani
Sajili/Futa:

Sajili na/au futa waasiliani kwa menyu za Faksi, Kwenye Kompyuta (Barua pepe), na Changanua kwa Folda/FTP ya Mtandao.

Mara kwa mara:

Sajili waasiliani wanaotumiwa mara kwa mara ili kuwafikia haraka. Pia unaweza kubadilisha mpangilio wa orodha.

Chapisha Waasiliani:

Chapisha anwani yako ya orodha.

Angalia Chaguo:

Badilisha jinsi orodha ya waasiliani inavyoonyeshwa.

Chaguo za Utafutaji:

Badilisha mbinu ya kutafuta waasiliani.

Nakili Kiwango Hisi cha Rangi:

Teua mpangilio wa unyeti wa kuthibitisha iwapo waraka ni wa monokromu au rangi unaponakili kwa kutumia Oto.

Unaweza kuteua unyeti kutoka kwenye viwango vitano kati ya B&W zaidi na Rangi zaidi.

Nyaraka huonekana kutambazwa katika monokromu unapoiteua karibu na B&W zaidi, na kwenye rangi unapoiteua karibu na Rangi zaidi.

Mapendekezo ya Kusafisha Kichanganuzi:

Teua Zima iwapo hutaki kuonyesha ujumbe unaokuarifu wakati wa kusafisha vijenzi vya utambazaji wa ADF.

Weka upya hesabu ya Ukurasa:

Inaweka upya jumla ya idadi ya kurasa za rangi na za rangi moja zilizohifadhiwa na kiolesura: mtandao Kamili, mtandao wa Ziada, na Nyingine.

Hata hivyo, jumla ya idadi ya uchapishaji na idadi ya kurasa zilizochapishwa na ukubwa wa karatasi haifai kuwekwa upya.

Idadi ya kurasa zilizochapishwa kutoka kwa kiolesura cha mtandao uliosakinishwa kwa hiari kinahesabiwa katika “Mtandao wa Ziada”, na idadi ya kurasa zilizochapishwa kutoka kwa kiolesura cha USB, faksi, nakala, n.k zinahesabiwa katika “Nyingine”.

Unaweza kuangalia idadi ya sasa ya kurasa zilizohifadhiwa kwenye Karatasi ya Historia ya Matumizi (Mipangilio > Hali ya Printa/Chapisha > Krtasi ya Historia Matumizi).

Ondoa Data ya Kumbukumbu ya Ndani:

Kipengee hiki kinaonyeshwa kwenye kichapishi patanifu cha PCL au PostScript.

Futa data ya kumbukumbu ya ndani ya kichapishi, kama vile fonti iliyopakuliwa na makro kwa uchapishaji wa PCL au kazi ya kuchapisha nenosiri.

Mipangilio ya Kufuta HDD:

Weka mipangilio ya kuchata data zilizohifadhiwa kwenye diski kuu ya ndani.

Kazi za kuchapisha, kunakili na kutambaza huhifadhiwa kwa muda kwenye diski kuu ili kushughulikia data ya uchapishaji ulioidhinishwa na kiwango kikubwa cha kunakili, kutambaza, kuchapisha n.k. Weka mipangilio ya kufuta data hii kwa usalama.

Mpangilio wa Kufuta Kukumbuku Kiotomati:

Ikuiwezeshwa, data lengwa hufutwa moja baada ya nyingine wakati si muhimu tena, kama vile wakati kuchapisha au kutambaza kumekamilika. Data lengwa inayofutwa ni data iliyoandikwa wakatika kitendaji kimewashwa.

Kwa sababu ni muhimu kuweza kufikia diski kuu, muda wa kuingiza modi ya kuokoa nishati utachelewa.

Futa Kumbukumbu Yote:

Futa data yote kwenye diski kuu. Unaweza kutekeleza utendaji mwingine au kuzima kifaa wakati wa kubadili umbizo.

  • Kasi ya Juu:

    Futa data yote kwa kutumia amri maalum ya kufuta.

  • Andika juu:

    Hufuta data yote kwa kutumia amri maalum ya kufuta, na kufuta data nyingine katika maeneo ya kufuta data.

  • Kuandikiza Mara Tatu:

    Hufuta data yote kwa kutumia amri maalum ya kufuta, na kufuta mara tatu data nyingine katika maeneo yote ya kufuta data.

Mipangilio ya Usalama:

Unaweza kuunda mipangilio ya usalama ifuatayo.

Vikwazo:

Toa kibali cha kubadilisha mipangilio ya vipengee vifuatavyo wakati kufuli la paneli limewezeshwa.

  • Ufikiaji wa kumbukumbu ya Kazi

  • Fikia ili uweze Kuwasajili/Kuwafuta Waasiliani

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Faksi

  • Ufikiaji wa Batli ya Usambazaji Faksi

  • Ufikiaji wa Ripoti ya Faksi

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Kuh. Cha. kwa Folda/FTP ya Mt'o

  • Ufikiaji wa hivi karibuni wa Changanua kwa Barua pepe

  • Ufikiaji wa Onyesha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe

  • Ufikiaji wa Chapisha Historia ya Zil'tumwa ya Cha. Barua pepe

  • Ufikiaji wa Lugha

  • Ufikiaji wa Karatasi Nyembamba

  • Ufikiaji wa Hali Tulivu

  • Ulinzi wa Data ya Kibinafsi

Fikia Vidhibiti:

Teua On ili kuzuia vipengele vya bidhaa. Hii huwahitaji watumiaji kuingia kwenye paneli dhibiti ya bidhaa kwa majina yao ya mtumiaji na nenosiri kabla waweze kutumia vipengele vya paneli dhibiti. Kwenye Kubali Kazi za Mtumiaji Asiyejulikana, unaweza kuteua iwapo utaruhusu kazi zisizo na maelezo yanayostahili ya uhalalishaji au la.

Mipangilio ya Msimamizi:
  • Nenosiri la Msimamizi

    Weka, badilisha, au ufute nenosiri la msimamizi.

  • Mpangilio wa Kufunga

    Teua kama utafunga paneli dhibiti au la kwa kutumia nenosiri lililosajiliwa katika Nenosiri la Msimamizi.

Ufichamishaji wa Nenosiri:

Teua On ili kusimba nywila yako kwa njia fiche. Unaweza pia kuunganisha kifaa cha USB ili iwe nakala rudufu ya ufunguo uliosimbwa fiche.

Batli ya Ukaguzi:

Teua On ili urekodi kumbukumbu ya ukaguzi.

Uthibitishaji wa Programu Inapoanza:

Teua On ili uthibitishe programu ya kichapishi unapoanzisha.

Utafiti wa Wateja:

Teua Idhinisha ili kutoa maelezo ya matumizi ya bidhaa kama vile idadi ya machapisho kwa Seiko Epson Corporation.

Rejeza Mipangilio Chaguo-msingi:

Weka upya mipangilio kwenye menyu zifuatazo katika changuo-msingi zake.

  • Mipangilio ya Mtandao

  • Nakili Mipangilio

  • Mip'o ya Ucha'uzi

  • Mipangilio ya Faksi

  • Ondoa Data na Mipangilio Yote

Sasisho la Pro.:

Unaweza kupata maelezo ya programu dhibiti kama vile toleo lako la sasa na maelezo kuhusu visasisho vinavyopatikana.

Sasisha:

Angalia iwapo toleo la sasa la programu dhibiti imepakiwa kwenye seva ya mtandao.Iwapo kisasisho kinapatikana, unaweza kuteua iwapo utaanza kusasisha au la.

Taarifa:

Teua On ili kupokea taarifa iwapo kisasisho cha programu dhibiti inapatikana.