Hufungua dirisha la Laiti ya Kipangaji cha Kazi. Hapa unaweza kufungua na kuhariri data iliyohifadhiwa awali.
Hufungua dirisha la EPSON Status Monitor 3. Unaweza kuthibitisha hali ya kichapishi na matumizi yake hapa. Unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki. Unaweza kuipakua kutoka kwenye tovuti ya Epson.
Hukuruhusu kuunda mipangilio kwa vipengee kwenye dirisha la EPSON Status Monitor 3. Unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuwezesha kipengele hiki. Unaweza kuipakua kutoka kwenye tovuti ya Epson.
Hukuruhusu kuunda mipangilio mbalimbali. Bofya kulia kila kipengee ili kuona Msaada kwa maelezo zaidi.
Huonyesha kazi zinazosubiri kuchapishwa. Unaweza kuangalia, kusitisha, au kuendelea na kazi za kuchapisha.
Huonyesha idadi ya laha za karatasi zilizoingizwa kwenye kichapishi au ADF. Unahitaji kusakinisha EPSON Status Monitor 3 ili kuangalia jumla ya idadi ya laha. Unaweza kuipakua kutoka kwenye tovuti ya Epson.
Hubadilisha lugha ya kutumiwa kwenye dirisha la kiendeshi cha kichapishi. Ili kutekeleza mipangilio, funga kiendeshi cha kichapishi, na kisha ukifungue tena.