Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Huwezi kubadilisha mipangilio iliyozuiwa na msimamizi wako.
Teua chanzo cha karatasi ili kubainisha ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyopakia. Wakati Uk. Karat'i Tambua Otomatiki iimewezeshwa, kichapishi hugundua ukubwa wa karatasi uliyopakia.
Teua On ili kutoa kipaumbele uchapishaji wa karatasi iliyopakiwa kwenye mpenyo wa mlisho wa karatasi.
Teua On Ili kuweka karatasi kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa A4 wakati hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa kama Letter, au huweka kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa Letter ambapo hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa A4.
Wakati karatasi zinaisha, karatasi inaingizwa kiotomatiki kutoka kwa chanzo cha karatasi chenye mipangilio sawa na mipangilio ya karatasi ya kazi za uchapisahaji. Unaweza kuweka uchaguaji otomatiki wa kila chanzo cha karatasi kwa kila kipengele katika kazi ya kunakili, faksi, au nyingine. Huwezi kuzima kila kitu.
Mpangilio huu unalemazwa unapochagua chanzo maalum cha karatasi katika mipangilio ya karatasi ya kazi za uchapishaji. Kulingana na mpangilo wa aina ya karatasi ulio kwenye kichupo Kuu cha kiendeshi cha printa, karatasi inaweza kuingizwa kiotomatiki.
Teua On ili kuonyesha ujumbe wa kosa wakati ukubwa wa karatasi ulioteuliwa haufanani na karatasi iliyopakiwa.
Mipangilio hii ya chapisho inatumiwa wakati unachapisha kwa kutumia kifaa cha nje bila kutumia kiendeshi cha kichapishaji. Mipangilio hii ya chapisho inatumiwa wakati unachapisha kwa kutumia kiendeshi cha kichapishaji.
Rekebisha pambizo ya juu ya karatasi.
Rekebisha pambizo ya kushoto ya karatasi.
Rekebisha pambizo ya juu ya ukurasa wa nyuma wakati unatekeleza uchapishaji wa pande 2.
Rekebisha pambizo ya kushoto ya ukurasa wa nyuma wakati unatekeleza uchapishaji wa pande 2.
Teua On ili kuangalia upana wa karatasi kabla ya kuchapisha. Hii huzuia uchapishaji nje ya mipaka ya karatasi wakati mpangilio wa ukubwa wa karatasi sio sahihi, lakini hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Huruka kurasa tupu katika data ya uchapishaji kiotomatiki.
Weka mipangilio kama ya uangavu na ubainifu, na utekeleze marekebisho ya rangi unapochapisha kutoka kwenye kifaa cha nje. Kipengele hiki kikiwashwa, mipangilio ya marekebisho ya rangi ya kichapishi inatawala mipangilio ya kiendeshi cha kichapishi cha kawaida.
Ung’avu
Ulinganuzi
Kulowesha
Uwiano Mwekundu
Uwiano wa Kijani
Uwiano wa Bluu
Teua chaguo za Usanidi wa Chapa ya PDL unazotaka kwa PCL au uchapishaji cha PostScript.
Ukubwa wa Karatasi
Teua ukubwa chaguo-msingi wa karatasi kwa uchapishaji wa PCL au PostScript.
Aina ya Karatasi
Teua aina chaguop-msingi wa karatasi kwa uchapishaji wa PCL au PostScript.
Mwelekeo
Teua uelekeo chaguo-msingi kwa uchapishaji wa PCL au PostScript.
Ubora
Teua ubora wa chapisho chapishaji wa PCL au PostScript.
Hali ya Kuokoa Wino
Teua On ili kuhifadhi kiungo kwa kupunguza uzito wa chapisho.
Agizo la Chapa
Ukurasa wa Mwisho Juu
Huanza kuchapisha kutoka kwenye ukurasa wa kwanza wa faili.
Ukurasa wa Kwanza Juu
Huanza kuchapisha kutoka kwa ukurasa wa mwisho wa faili.
Idadi ya Nakala
Weka idadi ya nakala za kuchapisha.
Pambizo ya Kufunga
Teua mwelekeo wa kuweka pamoja.
Utemaji Otomati wa Karatasi
Teua On ili kuondoa karatasi kiotomatiki uchapishaji unapokoma wakati wa kazi ya kuchapisha.
Uchapishaji wa Pande 2
Teua On ili kutekeleza uchapishaji wa pande 2.
Chanzo cha Fonti
Mkazi
Teua ili kutumia fonti iliyosakinishwa awali kwenye kichapishi.
Pakua
Teua kutumia fonti uliyopakua.
Nambari ya Fonti
Teua nambari chaguo-msingi ya fonti kwa chanzo cha fonti chaguo-msingi. Nambari inayopatikana hutofautiana kulingana na mipangilio uliyoweka.
Giza
Weka toni ya fonti chaguo-msingi iwapo fonti inaweza kupimwa na ina toni isiyobadilika. Unaweza kuteua kutoka cpi 0.44 hadi 99.99 (vibambo kwa kila inchi), kwa nyongeza ya 0.01.
Kipengee hiki huenda kisionekane kulingana na mipangilio ya chanzo cha fonti au nambari ya fonti.
Urefu
Weka urefu wa chaguo-msingi ya fonti iwapo fonti inaweza kupimwa au inawiana. Unaweza kuteua kutoka alama 4.00 hadi 999.75, kwa nyongeza ya 0.25.
Kipengee hiki huenda kisionekane kulingana na mipangilio ya chanzo cha fonti au nambari ya fonti.
Seti ya Alama
Teua seti ya ishara chaguo-msingi ya ishara. Iwapo fonti uliyoteua kwenye mipangilio ya chanzo cha fonti na nambari ya fonti haipatikani kwenye mipangilio ya seti mpya ya ishara, mipangilio ya chanzo cha fonti na nambari ya fonti inabadilishwa kiotomatiki kwa thamani chaguo-msingi, IBM-US.
Fomu
Weka idadi ya mistari kwa ukubwa na mwelekeo wa karatasi iliyoteuliwa. Hii pia husababisha mabadiliko ya uwekaji nafasi ya mstari (VMI), na thamani mpya ya VMI inahifadhiwa kwenye kichapishi. Hii humaanisha kuwa mabadiliko ya baadaye katika mipangilio ya ukubwa na mwelekeo wa karatasi inasababisha mabadiliko kwenye thamani ya Fomu kulingana na VMI iliyohifadhiwa.
Kitendaji cha CR
Teua amri ya kuingiza mstari unapochapisha kwa kiendeshi kutoka kwenye mfumo bainifu wa uendeshaji.
Kitendaji cha LF
Teua amri ya kuingiza mstari unapochapisha kwa kiendeshi kutoka kwenye mfumo bainifu wa uendeshaji.
Upang. Chanzo cha Karatasi
Weka kazi kwa amri ya kuteua chanzo cha karatasi. Wakati 4 imeteuliwa, amri zimewekwa kama patanifu na HP LaserJet 4. Wakati 4K imeteuliwa, amri zimewekwa kama patanifu na HP LaserJet 4000, 5000, na 8000. Wakati 5S imeteuliwa, amri zimewekwa kama patanifu na HP LaserJet 5S.
Laha la Kosa
Teua On ili kuchapisha laha inayonyesha hali kosa linapotokea wakati wa uchapishaji wa PostScript au PDF.
Uwekaji rangi
Teua modi ya rangi kwa uchapishaji wa PostScript.
Jozi
Teua On wakati unachapisha data ambayo inajumuisha taswira mbili. Programu-tumizi inaweza kutuma data mbili hata iwapo mipangilio ya kiendeshi cha kichapishi imewekwa kwa ASCII, lakini unaweza kuchapisha data wakati kipengee hiki kimewezeshwa.
Ukubwa wa Ukurasa wa PDF
Teua ukubwa wa karatasi unapochapisha faili ya PDF. Iwapo Oto imeteuliwa, ukubwa wa karatasi unatambuliwa kulingana na ukubwa wa ukurasa wa kwanza.
Teua hatua ya kutekeleza wakati kosa la uchapishaji ya pande 2 linatokea au kosa la kujaa kwa kumbukumbu linapotokea.
On
Huonyesha tahadhari na vichapisho katika modi ya upande mmoja wakati kosa la uchapishaji wa pande 2 linatokea, au huchapisha kile kichapishi kinaweza kuchakata wakati kosa la kujaa kwa kumbukumbu linatokea.
Zima
Huonyesha ujumbe wa kosa na kukatisha uchapishaji.
Kifaa cha Kumbukumbu:
Teua Wezesha ili kuruhusu kichapishi kufikia kifaa cha kumbukumbu kilichochomekwa.Iwapo Lemaza imeteuliwa, huwezi kuhifadhi data kwenye kifaa cha kumbukumbu kwa kichapishi.Hii huzuia hati za siri dhidi ya kuondolewa kinyume cha sheria.
Kushiriki Faili:
Teua iwapo utatoa kibali cha kuandika kwenye kifaa cha kumbukumbu kutoka kwa kompyuta iliyounganishwa ya USB au kutoka kwa kompyuta iliyounganishwa ya mtandao.
Teua Washa ili kuzuia wino kumwagika kwenye machapisho yako, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Teua On ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji. Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi.
Teua muda wa kukausha wino unaotaka kutumia unapotekeleza uchapishaji wa pande 2.Kichapishi huchapisha upande mwingine baada ya kuchapisha upande mmoja.Iwapo chapisho lako limepakwa wino, ongeza mpangilio wa muda.
Teua Washa ili kubadilisha uelekeo wa chapisho; Huchapisha wakati kichwa cha chapisho kinasonga upande wa kushoto na kulia.Ikiwa mistari mlalo na wima kwenye nakala yako inaonekana kuwa ina ukungu au haijalinganishwa, kulemaza kipengele hiki kunaweza kutatiza tatizo hilo; hata hivyo, kufanya hivyo kunaweza kupunguza kasi ya chapa.
Teua Washa ili kurefusha kiotomatiki kishikilia auni ya karatasi towe unapochapisha kwenye karatasi ya ukubwa wa A4.
Teua Wezesha ili kuruhusu kompyuta kufikia kichapishi inapounganishwa kwenye USB. Wakati Lemaza imeteuliwa, uchapishaji na utambazaji ambao haujatumwa kupitia muunganisho wa mtandao unazuiwa.
Baibisha urefu wa muda katika sekunde ambazo lazima ukamilike kabla ya kuisha kwa mawasiliano ya USB kwa kompyuta baada ya kichapishi kupokea kazi ya chapisho kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi cha PostScript au kiendeshi cha kichapishi cha PCL. Iwapo kukamilika kwa kazi hakujabainishwa wazi kutoka kwa kiendeshi cha kichapishi cha PostScript au kiendeshi cha kichapishi cha PCL, inaweza kusababisha mawasiliano ya USB yasiyo na mwisho. Wakati hii inatokea, kichapishi kinakamilisha mawasiliano baada ya muda uliobainishwa kukamilika. Ingiza 0 (sufuri) iwapo hutaki kukamilisha mawasiliano.