Mipangilio Msingi

Mipangilio ya K'si:

Bainisha mipangilio ya chanzo cha karatasi ambayo unataka kuchapisha kwenye.

Punguza/Ongeza:

Husanidi mgao wa ukuzaji wa upanuaji au upunguzaji. Donoa thamani na ubainishe ukuzaji katika masafa ya 25 hadi 400%.

  • Mip. wakati Ime'iwa

    Hutumia mipangilio uliyoweka ya kuhifadhi kwenye hifadhi.

  • Otomatiki

    Hukuza au kupunguza data ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi ulioteua.

  • Pu. ili Itoshee Kar'i

    Huchapisha data katika ukubwa ndogo kuliko thamani ya Punguza/Ongeza ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi. Iwapo thamani ya Punguza/Ongeza ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi, huenda data ikachapishwa zaidi ya kingo za karatasi.

  • Saizi Halisi

    Huchapisha kwa ukuzaji wa 100%.

  • A3→A4 na nyingine

    Hukuza au kupunguza data kiotomatiki ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi bainifu.

Pande 2:

Teua muundo wa pande 2.

  • Pande 2

    Tuea iwapo unataka kuchapisha ukitumia pande 2 au la.

  • Kufunga

    Teua nafasi ya uunganishaji kwa uchapishaji wa pande 2.

Kurasa Nyingi:

Teua muundo wa kuchapisha.

  • Ukurasa Mmoja

    Huchapisha data ya pande moja kwenye laha moja.

  • 2-juu

    Huchapisha data mbili za upande mmoja kwenye laha moja katika muundo wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo.

  • 4-juu

    Huchapisha data nne za upande mmoja kwenye laha moja katika muundo wa 4-up. Teua mpangilio wa muundo.

Kumalizia:
  • Kumalizia

    Teua Pangiliza (Mpang'o wa Ukurasa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi zilizochanganywa kwa mpangilio na kupangwa kwenye vikundi. Teua Kikundi (Kurasa Sawa) ili kuchapisha nyaraka za kurasa nyingi kwa kupata kurasa zenye nambari sawa kama kikundi.

  • Toa Karatasi

    Iwapo utateua Geuza Mpangilio, unaweza kuchapisha kwa njia mbadala kwenye mwelekeo wa taswira na mwelekeo wa mandhari.

Kijitabu:

Bainisha mipangililo hii unapotaka kuunda kijitabu kutoka kwenye machapisho yako.

  • Kijitabu

    Hukuruhusu kuunda kijitabu kutoka kwenye machapisho yako.

  • Kufunga

    Teua nafasi ya uunganishaji wa kijitabu.

  • Pambizo ya Ufungaji

    Teua ukingo wa kuunganisha. Unaweza kuweka 0 hadi 50 mm kuwa ukingo wa uunganishaji kwa uongenezaji wa 1 mm.

  • Jalada

    Hukuruhusu kuongeza majalada kwenye kijitabu.

  • Mipangilio ya K'si

    Chagua chanzo cha karatasi ulichoweka karatasi kwa ajili ya majalada.

  • Jalada la Mbele

    Bainisha mipangilio ya uchapishaji ya jalada la mbele. Iwapo hutaki kuchapisha jalada la mbele, teua Usichapishe.

  • Jalada la Nyuma

    Bainisha mipangilio ya uchapishaji ya jalada la nyuma. Iwapo hutaki kuchapisha jalada la nyuma, teua Usichapishe.