Kwa kutegemea vipengee, mipangilio ambayo imechaguliwa wakati faili ilikuwa imehifadhiwa kwenye hifadhi bado itatumika kiotomatiki.
Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.
Teua umbizo la faili.
Unapotumia PDF, PDF/A au TIFF kama ubizo la faili, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).
Mgao wa Mfinyazo:
Teua kiwango cha kufinyaza picha iliyotambazwa.
Mipangiliuo ya PDF:
Unapoteua PDF kama mpangilio wa kuhifadhi umbizo, tumia mipangilio hii kulinda faili za PDF.
Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kufungua, weka Nenosiri la Kufungua Hati. Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kuchapisha au kuhariri, weka, Nenosiri la Vibali.
Teua upeo wa juu wa ukubwa wa faili ambayo inaweza kuambatishwa kwenye barua pepe.