> Kukarabati Kichapishi > Kuboresha Ubora wa Uchapishaji > Kusafisha Kijia cha Karatasi na Umwagikaji wa Wino

Kusafisha Kijia cha Karatasi na Umwagikaji wa Wino

Wakati uchapishaji una uchafu au kuchakaa, safisha rola iliyo ndani.

Muhimu:

Usitumie karatasi ya shashi kusafisha ndani ya kichapishi. Nozeli za kichwa cha kuchapisha zinaweza kuzibwa na nyuzi za pamba.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Usfshaji Mwongzo wa Krtasi.

  3. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kupakia karatasi na kusafisha njia ya karatasi.

  4. Rudia utaratibu huu hadi karatasi iwache kuchafuliwa na wino.