Kuleta cheti kilichotiwa Sahihi cha CA

Leta CA-signed Certificate ulichopata kwenye kichapishi.

Muhimu:
  • Hakikisha mpangilio wa tarehe na saa wa kitambazaji ni sahihi. Huenda cheti si halali.

  • Ukipata cheti ukitumia CSR iliyoundwa kutoka kwa Web Config, unaweza kuleta cheti mara moja.

  1. Weka anwani ya IP ya kichapishi katika kivinjari ili kufikia Web Config.

    Ingiza anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa kompyuta ambayo imeunganishwa kwenye mtandao sawa na wa kichapishi.

    Unaweza kuangalia anwani ya IP ya kichapishi kutoka kwa menyu inayofuata.

    Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio ya Mtandao > Hali ya Mtandao > Hali ya LAN ya waya/Wi-Fi

  2. Ingiza nenosiri la msimamizi ili kuingia kama msimamizi.

  3. Teua kwenye orodha inayofuata.

    kichupo cha Network Security > SSL/TLS > Certificate, au IPsec/IP Filtering > Client Certificate au IEEE802.1X

  4. Bofya Import

    Ukurasa wa kuleta cheti unafunguliwa.

  5. Ingiza thamani kwa kila kipengee. Weka CA Certificate 1 na CA Certificate 2 unapothibitisha njia ya cheti kwenye kivinjari cha wavuti kinachofikia kichapishi.

    Kwa kutegemea unapoundia CSR na umbizo la faili la cheti, mipangilio inayohtajika inaweza kutofautiana. Ingiza thamani kwa vipengee vinavyohitajika kulingana na yafuatayo.

    • Cheti cha umbizo la PEM/DER kilichopatikana kutoka Web Config
      • Private Key: Usisanidi kwa sababu kichapishi kina ufunguo wa kibinafsi.
      • Password: usisanidi.
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Cha hiari
    • Cheti cha umbizo la PEM/DER kilichopatikana kutoka kwenye kompyuta
      • Private Key: Unahitaji kuweka.
      • Password: usisanidi.
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Cha hiari
    • Cheti cha umbizo la PKCS#12 kilichopatikana kutoka kwenye kompyuta
      • Private Key: usisanidi.
      • Password: Cha hiari
      • CA Certificate 1/CA Certificate 2: Usisanidi.
  6. Bofya OK.

    Ujumbe wa kukamilisha unaonyeshwa.

Kumbuka:

Bofya Confirm ili uthibitishe maelezo ya cheti.