> Kutatua Matatizo > Haiwezi Kuchapisha > Programu au Kiendeshi cha Printa Hakifanyi Kazi Vizuri > Hakiwezi Kuchapisha Ingawa Muunganisho Umewekwa (Windows)

Hakiwezi Kuchapisha Ingawa Muunganisho Umewekwa (Windows)

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Kichapishi kinasubiri au kiko nje ya mtandao.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Ikiwa kichapishi kiko nje ya mtandao au kinasubiri, futa mpangilio wa nje ya mtandao au wa kusubiri kutoka kwa menyu ya Kichapishi.

Kuna tatizo na programu au data.

Suluhisho

  • Hakikisha umesakinisha kiendesha kichapishi halali cha Epson (EPSON XXXXX). Iwapo kiendeshi cha kichapishi cha Epson halali hakijasakinishwa, utendaji unaopatikana una kipimo. Tunapendekeza kutumia kiendeshi cha kichapishi cha Epson halali.

  • Ikiwa unachapisha picha yenye data kubwa, huenda komyuta ikakosa nafasi ya kutosha kwenye kumbukumbu. Chapisha picha kwa msongo wa chini au ukubwa mdogo.

  • Ikiwa umejaribu usuluhishaji wote na hujatatua tatizo hilo, jairbu kusakinusha na kisha usakinishe kiendeshi cha printa upya.

  • Unaweza kufuta tatizo kwa kusasisha programu hadi toleo la sasa. Ili kukagua hali ya programu, tuimia zana ya kusasisha programu.

Haiwezi kuchapisha kazi wakati nenosiri limewekwa kama ninatumia toleo la zamani la maunzi.

Suluhisho

Iwapo ujumbe ulio hapa chini utaonyeshwa kwenye kiendeshi cha kichapishi, sasisha maunzi ya kichapishi.

Iwapo huwezi kusasisha maunzi kwa sababu fulani, unaweza kuendelea kuchapisha kwa kiwango sawa cha usalama kama cha maunzi ya zamani.

Ili kuchapisha ukitumia maunzi ya zamani, tafadhali tekeleza mipangilio ifuatayo kwenye kiendeshi cha kichapishi.

Fungua kichupo cha Mipangilio ya Hiari katika sifa za kichapishi.

Bofya Mipangilio ya Kiendeshaji.

Teua Tumia Nenosiri Halali na ubofye SAWA.

Kuna tatizo na hali ya kichapishi.

Suluhisho

Bofya EPSON Status Monitor 3 kwenye kichupo cha kiendeshi cha kichapishi Utunzaji, na kisha uangalie hali ya kichapishi. Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uteue Wezesha EPSON Status Monitor 3.

Bado kuna shughuli inayosubiri kuchapishwa.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji. Iwapo data isiyohitajika itasalia, teua Katisha nyaraka zote kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Kichapishi hakijateuliwa kuwa kichapishi chaguomsingi.

Suluhisho

Bofya mara mbili kwenye aikoni katika Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi (au Vichapishi, Vichapishi na Faksi) kisha ubofye Weka kuwa kichapishi chaguomsingi.

Kumbuka:

Ikiwa kuna aikoni nyingi za vichapishi, angalia yafuatayo ili kuchagua printa sahihi.

Mfano)

Muunganisho wa USB: Misururu ya EPSON XXXX

Muunganisho wa mtandao: Misururu ya EPSON XXXX (mtandao)

Ukisakinisha kiendesha kichapishi mara nyingi, nakala za kiendesha kichapishi huweza kuundwa. Iwapo nakala kama vile “Misururu ya EPSON XXXX (nakala 1)” zinaundwa, bofya kulia ikoni ya kiendeshi kilichonakiliwa, na kisha ubofye Ondoa Kifaa.

Lango la kichapishi halijawekwa ipasavyo.

Suluhisho

Bofya Foleni ya U'haji kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

Hakikisha kwamba lango la kichapishi limewekwa ipasavyo jinsi inavyoonyeshwa hapa chini Sifa > Lango kutoka kwenye menyu ya Kichapishi.

Munganisho wa USB: USBXXX, Muunganisho wa Network: EpsonNet Print Port

Iwapo huwezi kubadilisha lango, chagua Endesha kama msimamizi kwenye menyu ya Kichapishi. Iwapo Endesha kama msimamizi haijaonyeshwa, wasiliana na msimamizi wako wa mfumo.