Kwa kutumia menyu hii, unaweza kudumisha bidhaa kama msimamizi wa mfumo. Pia hukuruhusu kuzuia vipengele vya bidhaa kwa watumiaji binafsi ili kukidhi kazi yako au mtindo wa ofisi.
Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Usimamizi wa Mtandao
Usimamizi wa Mtandao
Usafishaji wa Mara kwa Mara
Wezesha mpangilio huu ili kufanya usafishaji wa kichwa kila mara wakati idadi fulani ya kurasa zimechapishwa au kichapishi kimegundua kuwa usafishaji wa kichwa ni muhimu. Teua chochote tofauti na Zima ili kudumisha ubora unaostahili wa chapisho. Chini ya hali kama hizi, tekeleza Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa na Usafishaji Kichwa cha Chapa mwenyewe.
Matatizo ya uchapishaji
Wakati Zima imeteuliwa kwa Usafishaji wa Mara kwa Mara
Unapochapisha kwa ubora wa juu, kama vile picha
Zima
Hulemaza usafishaji wa kichwa wa kila kipindi.
Baada ya Kuchapisha
Husafisha kichwa kila mara wakati ambapo uchapishaji umekamilika.
Ratiba
Hufanya usafishaji wa mara kwa mara wakati ambapo ulibainisha.
Iwapo kichapishi kimezimwa wakati maalum, usafishaji kichwa kila mara hufanywa wakati ambapo kichapishi kimewashwa.
Ondoa Data ya Kumbukumbu ya Ndani
Kipengee kinaonyeshwa kwenye kichapishi kinachoambatana na PCL au PostScript.
Futa data ya kumbukumbu ya ndani ya kichapishi, kama vile fonti iliyopakuliwa na makro ya uchapishaji wa PCL.
Fonti ya PDL, Makro, na Eneo la Kufanyia kazi
Kipengee kinaonyeshwa kwenye kichapishi kinachoambatana na PCL au PostScript.
Futa data ya kumbukumbu ya ndani ya kichapishi, kama vile fonti iliyopakuliwa na makro ya uchapishaji wa PCL.
Futa Kazi Zote za Kumb. Ndani
Futa data ya kumbukumbu ya ndani ya kichapishi, kama vile kazi na manenosiri.
Mipangilio ya Usalama
Mipangilio ya Msimamizi
Nenosiri la Msimamizi
Weka, badilisha, au ufute nenosiri la msimamizi.
Mpangilio wa Kufunga
Teua kama utafunga paneli dhibiti au la kwa kutumia nenosiri lililosajiliwa katika Nenosiri la Msimamizi.
Ufichamishaji wa Nenosiri
Teua On ili kusimba nywila yako kwa njia fiche. Ukibonyeza kitufe cha kuzima wakati kinaendelea kuanzisha upya, data inaweza kuharibiwa na mipangilio ya kichapishi itarejeshwa kwa chaguomsingi lao. Hii ikifanyika, weka maelezo ya nenosiri tena.
Batli ya Ukaguzi
Teua On ili urekodi kumbukumbu ya ukaguzi.
Uthibitishaji wa Programu Inapoanza
Teua On ili uthibitishe programu ya kichapishi unapoanzisha.
Utafiti wa Wateja
Iwapo utakubali kutoa taarifa ya matumizi ya mteja, taarifa ya matumizi ya bidhaa kama vile idadi ya machapisho itatolewa kwa Seiko Epson Corporation.
Taarifa iliyokusanywa inatumika kuboresha bidhaa na huduma zetu.
Tupatie data yako ya matumizi
Huonyesha kama umekubali kutoa taarifa yako ya matumizi ya mteja au la.
Nchi/Eneo
Huonyesha nchi au eneo ambapo unatumia bidhaa iwapo umekubali kutoa taarifa yako ya matumizi ya mteja.
Rejeza Mipangilio Chaguo-msingi
Mipangilio ya Mtandao
Huweka upya mpangilio wa mtandao kwa chaguo msingi.
Zote isipokuwa Mipangilio ya Mtandao
Hurejesha mipangilio yote isispokuwa ya mipangilio ya mtandao kwa changuomsingi zao.
Mipangilio Yote
Hufuta maelezo yote ya kibinafsi yaliyohifadhiwa kwenye kumbukumbu ya printa na kuweka upya mipangilio yote kwa chaguo msingi wao.
Sasisho la Pro.
Unaweza kupata maelezo ya programu dhibiti kama vile toleo lako la sasa na maelezo kuhusu visasisho vinavyopatikana.
Sasisha
Husasisha programu maunzi moja kwa moja.
Sasisho Otomatiki la Programu
Sasisho Otomatiki la Programu
Teua On ili kusasisha programu maunzi otomatiki na kuweka siku ya wiki/saa ya kuanza ili usasishe.
Siku
Teua siku ya wiki ambapo unataka kusasisha programu maunzi.
Muda
Weka saa ambapo unataka kuanza kusasisha programu maunzi.
Taarifa
Teua On ili kuonyesha ikoni sasisho la programu maunzi kwenye skrini ya mwanzo.