> Kukarabati Kichapishi > Kuboresha Ubora wa Uchapishaji > Kurekebisha Ubora wa Chapisho

Kurekebisha Ubora wa Chapisho

Iwapo utagundua mistari wima isiyopangwa vizuri, taswira zisizoonekana vizuri, au mistari mlalo inayoonekana kwa umbali, rekebisha ubora wa chapisho. Iwapo unataka kurekebisha ubora wa chapisho kwa karatasi, kwanza unda mpangilio huu.

  1. Weka karatasi tupu yenye ukubwa wa A4 katika kichapishi.

  2. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.

  4. Fuata maagizo kwenye skrini ili kuchapisha ruwaza ya mpangilio wa kichwa cha chapisho, na kisha pangilia kichwa cha kuchapisha.

    • Ruwaza hii huekuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo machapisho yako hayaonekani vizuri.
      Tafuta na uteue nambari ya ruwaza imara zaidi.
    • Ruwaza hii hurukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo mistari wima iliyopigiliwa itaonekana kutopangiliwa vizuri.
      Tafuta na uteue idadi ya ruwaza ambayo ina mstari michache wima isiyopangiliwa vizuri.
    • Ruwaza hii hukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo utaona mistari mlalo inayoonekana kwa mbali katika vipindi vya muda wa kawaida.
      Tafuta na uingize nambari ya ruwaza iliyogawanywa na inayopindana.