> Kukarabati Kichapishi > Kuboresha Ubora wa Uchapishaji > Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha

Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha

Ikiwa nozeli zimeziba, chapa huwa hafifu au kuna mstari unaonekana. Ikiwa nozeli zimeziba sana, karatasi tupu itachapishwa. Wakati ubora wa chapisho umepungua, kwanza tumia kipengele cha kukagua nozeli na ukague kama nozeli zimeziba. Ikiwa nozeli zimeziba, safisha kichwa cha kuchapisha.

Muhimu:
  • Usifungue kifuniko cha wino au zima kichapishi wakati wa kusafisha kichwa. Ikiwa usafisha wa kichwa haujakamilika, huenda usiweze kuchapisha.

  • Kusafisha kichwa hutumia wino mwingi na unapaswa kufanywa ikiwa ni muhimu tu.

  • Wakati wino ni kidogo, huenda usiweze kusafisha kichwa cha kuchapisha.

  • Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha mara 3, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha, angalia nozeli tena, na kisha urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi kwa kutumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujakuwa bora, wasiliana na usaidizi wa Epson.

  • Ili kuzuia kichwa cha kuchapisha kisikaue, usichomoe printa wakati nishati imewashwa.

Unaweza kuangalia na kusafisha kichwa cha kuchapisha kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa.

  3. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kupakia karatasi na kuchapisha ruwaza ya kukagua nozeli.

  4. Chunguza muundo uliochapishwa.

    • Iwapo kuna mistari iliyotengana au sehemu zinazokosekana kama ilivyooshwa kwenye ruwaza ya “NG”, huenda nozeli za kichwa cha uchapishaji imeziba. Nenda kwa hatua inayofuata.
    • Iwapo huwezi kuona mistari ya vitone au sehemu inayokosekana kama kwenye ruwaza inayofuata “SAWA”, nozeli haijaziba. Usafishaji wa kichwa cha kichapishi si muhimu. Teua ili kutoka.
  5. Teua .

  6. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini kusafisha kichwa cha uchapishaji.

  7. Wakati usafishaji umekamilika, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli tena. Rudia usafishaji na uchapishaji hadi mistari yote ichapishwe kabisa.

Kumbuka:

Unaweza kuangalia na kusafisha kichwa cha kuchapisha kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi.

  • Windows

    Bofya Ukaguzi wa Nozeli ya Kichwa cha Kuchapisha kwenye kichupo cha Utunzaji.

  • Mac OS

    Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishaji > Ukaguzi wa Nozeli ya Kichwa cha Kuchapisha