Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.
Onyesha Mipangilio/Ficha Mipangilio
Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi. Unaweza kuonyesha au kuficha skrini ya sasa ya orodha ya mipangilio.
Rejesha Chaguo-msingi
Rejesha mipangilio yote katika thamani chaguomsingi za kiwanda. Mipangilio kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi pia hurejeshwa katika chaguomsingi zao.
Viwango vya Wino
Huonyesha kiwango kinachokadiriwa cha wino.
Chanzo cha K'tasi
Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Teua Uteuzi Otomatiki ili kuteua kiotomatiki chanzo cha karatasi kilichoteuliwa kwenye mipangilio ya kichapishi.
Ukubwa wa Waraka
Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na kimo cha karatasi kisha usajili ukubwa.
Mwelekeo
Teua mwelekeo unaotaka kutumia ili kuchapisha.
Aina ya Krtasi
Teua aina ya karatasi unayochapisha.
Ubora
Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Mipangilio inayopatikana inalinganana aina ya karatasi unayoteua. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.
Uchapishaji wa Pande 2
Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.
Settings
Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha. Unapochapisha nyaraka za kurasa nyingi, unaweza kuteua kuchapisha kuanzia upande wa mbele au upande wa nyuma wa ukurasa.
Uzito wa Uchapishaji
Teua aina ya waraka ili kurekebisha uzito wa chapisho. Iwapo uzito wa chapisho unaofaa umeteuliwa, unaweza kuzuia picha kutokea upande wa nyuma. Teua Mtumiaji-Amefafanuliwa ili kurekebisha uzito wa chapisho kikuli.
Kurasa Nyingi
Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya mpangilio wa muundo ili kubainisha utaratibu ambao kurasa zinachapishwa.
Copies
Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.
Pangiliza
Huchapisha nyaraka nyingi zilizolinganishwa kwa utaratibu na kupangwa kwenye vikundi.
Mpangilio Kinyume
Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.
Modi Tulivu
Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Uhakiki wa Chapisho
Huonyesha uhakiki wa waraka wako kabla ya kuchapisha.
Laiti ya Kipangaji cha Kazi
Kipengele cha Job Arranger Lite hukuruhusu kujumuisha faili mbalimbali zilizoundwa na programu tofuti na uzichapishe kama kazi moja ya uchapishaji.