> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Hali ya Kazi Usanidi wa Skrini

Hali ya Kazi Usanidi wa Skrini

Bonyeza kitufe cha ili kuonyesha menyu ya Hali ya Kazi. Unaweza kukagua hali kichapishi au kazi.

Hubadili orodha zilizoonyeshwa.

Chuja kazi kwa utendaji.

Wakati Inatumika imeteuliwa, huonyesha orodha ya kazi zinazoendelea na kazi zinazosubiri kuchakatwa.

Wakati Kumbukumbu imeteuliwa, huonyesha historia ya kazi.

Unaweza kukatisha kazi au kukagua msimbo wa kosa ulioonyeshwa kwenye historia wakati kazi imeshindikana.

Huonyesha makosa yoyote ambayo yametokea kwenye kichapishi. Teua kosa kutoka kwenye orodha ili kuonyesha ujumbe wa kosa.

Huonyesha makadirio ya kiwango cha wino.

Huonyesha makadirio ya maisha ya huduma ya kikasha cha ukarabati.

Inaonyesha makadirio ya matumizi ya nishati.

Kiwango cha nishati kilichoonyeshwa ni thamani ya mwongozo wa matumizi ya jumla na kinaweza kuwa tofauti kutegemea unavyotumia kipengee hiki.

Kinahesabiwa kwa kutumia fomula inayofuata.

<Kiwango cha nishati kinachohitajika kuchapisha kwenye ukurasa mmoja wa karatasi * kwa bidhaa hii>×<Idadi ya kurasa zilizochapishwa katika siku 7 zilizopita>

Tazama ufafanuzi unaofuata kwa maelezo kuhusu matumizi ya nishati ya bidhaa fulani.

* Data iliyotumika kuchapisha ukurasa moja wa karatasi ndiyo data ya kipimo cha kiwango cha TEC ya ISO / IEC10561 1999 ya muundo wa kipimo cha A.

Kuhusu matumizi ya nishati ya bidhaa fulani

Thamani ya TEC*1 ya bidhaa hii ni takriban 1/2 ya thamani ya kawaida*2 kuunganisha Programu ya Nyota ya Nishati ya Kimataifa.

*1 TEC ni kifupisho cha matumizi ya Umeme Kawaida na ndiyo matumizi ya nishati (kWh) kwa wiki kamili (siku 5 za uendeshaji uliorudiwa na kulala / kuzima + siku 2 za kulala / kuzima). Kiwango hiki kinatumika kama kiwango cha marejeleo kufuata “Programu ya Kimataifa ya Nyota ya Nishati”.

Thamani ya TEC ya bidhaa hii inakokotolewa kivyake na Epson kutegemea kiwango cha TEC cha mbinu ya kipimo cha Programu ya Kimataifa ya Nyota ya Nishati. Angalia tovuti ya Epson au wasiliana na usaidizi wa Epson kwa thamani ya TEC ya bidhaa hii na hali yake ya kipimo.

*2 Viwango kamili vya kuendana na Programu ya Kimataifa ya Nyota ya Nishati vimewekwa ili 25% bora ya bidhaa zenye utendaji bora wa kuhifadhi nishati kuendana na kiwango hiki.