Baadhi ya vipengee haviwezi kupatikana kulingana na mbinu ya kuchanganua uliyochagua au mipangilio mingine uliyoweka.
Chaguo za Menyu za Utambazaji
Hali ya Rangi
Teua iwapo utatambaza kwenye rangi au katika monokromu.
Umbizo la Faili
Teua umbizo ambalo unataka kuhifadhi taswira zilizotambazwa.
Unapotaka kuhifadhi kama PDF, PDF/A au TIFF, teua iwapo utahifadhi nakala zote asili kama faili moja (kurasa-nyingi) au uhifadhi kila nakala asili pekee yake (ukurasa mmoja).
Mgao wa Mfinyazo:
Teua kiwango cha kufinyaza picha iliyotambazwa.
Mipangiliuo ya PDF:
Unapoteua PDF kama mpangilio wa kuhifadhi umbizo, tumia mipangilio hii kulinda faili za PDF.
Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kufungua, weka Nenosiri la Kufungua Hati. Ili kuunda faili ya PDF ambayo inahitaji nywila wakati wa kuchapisha au kuhariri, weka, Nenosiri la Vibali.
Mwonekano
Teua mwonekano wa utambazaji.
Pande 2
Tambaza pande zote za nakala asili.
Mwelekeo (Asili):
Teua mwelekeo wa nakala asili.
Ufungaji(Asili):
Teua mwelekeo wa kuweka pamoja wa nakala asili.
Eneo la Kutambaza
Teua eneo la kutambaza. Ili kupuna nafasi nyeupe kwenye matini au taswira unapotambaza, teua Upunuaji Otomatiki. Ili kutambaza katika eneo nzima ya glasi ya kitambazaji, teua Upeo wa Eneo.
Mwelekeo (Asili):
Teua mwelekeo wa nakala asili.
Aina Asili
Teua aina ya nakala yako asili.
Mwelekeo (Asili)
Teua mwelekeo wa nakala asili.
Uzito
Teua ulinganuzi wa taswira iliyotambazwa.
Ondoa Kivuli
Ondoa vivuli vya nakala asili ya ambavyo vinaonekana katika taswira iliyotambazwa.
Fremu:
Ondoa vivuli katika ukingo wa nakala asili.
Katikati:
Ondoa vivuli vya pambizo za kuweka pamoja vya kijitabu.
Ond. Mas'o ya Panchi
Ondoa mashimo ya panji ambayo yanaonekana kwenye taswira iliyotambazwa. Unaweza kubainisha eneo la kufuta mashimo ya panji kwa kuingiza thamani kwenye kikasha upande wa kulia.
Mkao wa Kufuta:
Teua mkao ili kuondoa mashimo.
Mwelekeo (Asili):
Teua mwelekeo wa nakala asili.
Mada
Ingiza mada ya barua pepe katika vibambo vya alfanumeriki na alama.
Upeo wa Ukubwa wa Kiambatisho
Teua upeo wa juu wa ukubwa wa faili ambayo inaweza kuambatishwa kwenye barua pepe.
Jina la Faili
Kiambishi awali cha Jina la faili:
Ingiza kiambishi awali cha jina la taswira katika vibambo vya alfanumeriki na alama.