Iwapo utagundua mistari wima isiyopangwa vizuri, taswira zisizoonekana vizuri, au mistari mlalo inayoonekana kwa umbali, rekebisha ubora wa chapisho.
Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Teua Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.
Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini kuchapisha ruwaza ya upangiliaji na uitambaze.
Marekebisho hufanyika otomatiki.
Ikiwa ubora wa uchapishaji hautakuwa bora, ujumbe wa kuchapisha karatasi ya ukarabati unaonyeshwa kwenye paneli dhibiti. Nenda kwa hatua inayofuata.
Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuchapisha karatasi ya ukaguzi wa ukarabati.
Angalia kila ruwaza ili kufanya marekebisho.