> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Usanidi wa Skrini ya Nyumbani

Hii inaonyeshwa wakati programu maunzi inapatikana.

Donoa ili kusasisha programu maunzi ili kuboresha vipengele vya kichapishi. Tunapendekeza kutumia kichapishi na toleo la hivi karibuni zaidi la programu maunzi.

Huonyesha skrini ya Hali ya Printa.

Unaweza kuangalia kiwango cha wino na kiwango cha maisha ya huduma ya kisanduku cha matengenezo.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Mwongozo kwa Aikoni ya Mtandao

Huonyesha skrini ya Mipangilio ya Sauti ya Kifaa.

Unaweza kuweka Nyamazisha na Hali Tulivu. Pia unaweza kufikia menyu ya Sauti kutoka kwenye skrini. Unaweza pia kuweka mpangilio huu kutoka kwenye menyu ya Mipangilio.

Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi > Sauti

Huonyesha iwapo Hali Tulivu imewekwa kwa kichapishi au la. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho.

Huonyesha kuwa Nyamazisha imewekwa kwa kichapishi.

Teua ikoni ili kuingiza modi ya kusinzia. Wakati ikoni imewekewa rangi ya kijivu, kichapishi hakiwezi kuingiza modi ya kusinzia.

Huonyesha skrini ya Maelezo ya Data ya Faksi. Nambari inayoonyeshwa inaashiria idadi ya faksi ambazo bado hujasoma, kuchapisha au kuhifadhi.

Huonyesha kila menyu.

  • Nakili

    Hukuruhusu kunakili nyaraka.

  • Changanua

    Hukuruhusu kutambaza nyaraka na kuzihifadhi kwenye kifaa cha kumbukumbu au kompyuta.

  • Faksi

    Hukuruhusu kutuma faksi.

  • Zili'a Kabla

    Hukuruhusu kusajili mipangilio inayotumika mara kwa mara kunakili, kutambaza au kutuma faksi kama uwekaji awali.

  • Kifaa cha Kumbukumbu

    Hukuruhusu kuchapisha data ya JPEG, TIFF au PDF kwenye kifaa cha kumbukumbu kama vile kifaa cha USB kilichounganishwa kwenye kichapishi.

  • Kasha la Faksi

    Hukuruhusu kuhifadhi hati zilizopokelewa, hati za kutuma au hati kwa ajili ya kutuma faksi.

  • Chapisha Kutoka Kumb'u Ndani

    Hukuruhusu kuhifadhi kazi zilizotumwa kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi hadi kwenye kumbukumbu ya kichapishi kwa muda kabla ya kuchapisha. Unaweza kuchapisha kazi iliyolindwa kwa nenosiri na kuweka machapisho ya jaribio unapochapisha nakala nyingi.

  • Matengenezo

    Huonyesha menyu zinazopendekezwa kuimarisha ubora wa machapisho yako kama vile kuzibua nozeli kwa kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli na kutekeleza usafishaji wa kichwa, na kuboresha ukungu au mistari kwenye machapisho yako kwa kupangilia kichwa cha kuchapisha. Unaweza pia kuweka mpangilio huu kutoka kwenye menyu ya Mipangilio.

    Mipangilio > Matengenezo

  • Mipangilio

    Hukuruhusu kuweka mipangilio inayohusiana na udumishaji, mipangilio ya kichapishi na operesheni.

Kazi/Hali

Huonyesha kazi zinazoendelea zinazosubiri. Donoa ili kuonyesha aina ya kazi, kipima muda wa kuwasili, majina ya mtumiaji, nakadhalika kama orodha. Nambari inayoonyeshwa huashiria idadi ya kazi zinazosubiri.

Hutelezesha skrini upande wa kulia.